Na Mwandishi maalum.
LIGI Darajala la Pili Mkoa wa Dar es Salaam , hatua ya sita bora imezidi
kushika kasi ambapo hadi sasa timu ya Red Coast inaongoza ligi hiyo kwa
kujikusanyia pointi 7 baada ya kucheza mechi tatu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mharizo, Red Coast imejikusanyia pointi
hizo baada ya kuzifunga Abajalo
bao 1-0, huku ikilazimishwa sare ya bila
kufungana na Friends Rangers na jana Jumatatu iliichapa Sharif mabao 3-1,
katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Airwing.
Friends Rangers wanashika nafasi ya pili kwa
kuwa na pointi 5, ilizozivuna kwa kutoka sare ya bila kufungana na Day Break
katika mechi ya kwanza, kasha kulazimishwa tena sare ya bila kufungana na Red Coast na jana Jumatau
iliifunga Boom FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa.
Abajao inashiaka nafasi ya tatu ikiwa na pointi
4, huku Sharif Star ikishika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 3, ikifuatiwa na
Day Break yenye pointi 3 wakati Boom FC ikiburuza mkia kwa kuwa na pointi 1.
Kesho Jumatano ligi itaendelea kwa michezo
mitatu, Abajalo vs Friends Rangers uwanja wa Kinesi, Red Coast
vs Boom uwanja wa Makurumla na Sharif Stars vs Day Break uwanja wa Airwing. Ligi hiyo inatazamiwa kumalizika Aprili 27 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment