Aina mpya ya viini sugu vinavyosababisha Malaria na
ambavyo havisikii dawa vimegunduliwa na wanasayansi.
Watafiti wamevigundua viini hivyo Magharibi mwa Cambodia na
wanasema kuwa vina umbo tofauti la genetiki ikilinganishwa na viini vingine
duniani.
Viini hivi ni sugu kiasi cha kutosikia dawa
aina ya Artemisinin, dawa yenye nguvu zaidi katika kutibu Malaria.
Taarifa
ya kwanza kuwa wagonjwa walikuwa hawatibiki na dawa hiyo ilitokea mwaka 2008.
Tatizo hilo tangu hapo limeenea katika maeneo
mengine ya Asia ya Kusini.
Utafiti
huu umechapishwa katika jarida la ''Nature Genetics.''
Mtafiti
mkuu Daktari Olivo Miotto, wa chuo kikuu cha Oxford na kile cha Mahidol nchini
Thailand,amesema kuwa dawa zote zenye uwezo wa kuua Malaria na ambazo
zimevumbuliwa katika miaka ya hivi karibuni, zimekuwa ovyo katika kutibu
Malaria.
"Dawa
ya Artemisinin kwa sasa inafanya kazi vyema. Ndio silaha nzuri zaidi dhidi ya
ugonjwa huo na tunahitaji kuendelea kuitumia,'' alisema Daktari Miotto
Magharibi
mwa Cambodia kumetajwa kama sehemu yenye Malaria sugu.
Haileweki
ni kwa nini tangu mapema miaka ya 1950, viini vya Malaria katika eneo hilo , vimekuwa sugu.
Tatizo hilo pia limesambaa hadi katika sehemu
kadhaa za Asia na Afrika.
Kwa
sasa wanasayansi wana wasiwasi kuwa hali sawa na hiyo itajitokeza kwa dawa ya
Artemisinin. Dawa hiyo inatumika kote duniani kukabiliana na Malaria, na
inaweza kutibu ugonjwa kwa siku chache tu ikiwa itatumika na mchanganyiko wa
dawa zengine.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment