Mbunge mwingine yeye amesimamishwa kwa muda wa miezi mitatu
kwa sababu za ulevi.Katibu mkuu wa chama hicho Amama Mbabazi anasema hii kwa
tafsiri yake inamaanisha kuwa wabunge hao wamepoteza viti vyao, jambo ambalo
wahusika wanapinga.
Katibu mkuu wa chama tawala cha NRM na wakati
huo waziri Mkuu wa Uganda ,Amama
Mbabazi, ametangaza maamuuzi ya kamati kuu ya chama hicho kuhusu majaliwa ya
wabunge wanne waliopewa jina la ‘wabunge waasi’ kutokana na misimamo yao dhidi ya masuala
mbalimbali katika chama hicho.
Mbabazi
alitoa kauli hiyo na kusema, ''Muhammad Nsereko afukuzwe kutoka NRM;kuwa
Theodor Sekikubo afukuzwe kutoka NRM;kuwa Barnabas Tinkasimire afukuzwe kutoka
NRM;kuwa Wilfred Nuwagaba wamefukuzwe kutoka NRM; na kuwa Vicent Kyamadidi Muzuni
asimamishwe uana chama wa NRM kwa muda wa miezi mitatu.''
Wabunge
wanne waliofukuzwa kutoka chama:Nsereko;Sekikubo;Tinkasimire pamoja na Niwagaba
wamekuwa wakipinga na kukosoa saana uongozi wa sasa wa chama hususan kutokana
na madai ya ufisadi dhidi ya vigogo wa chama.
Na
wanasema hatua hii ni ya kuwaandama kisiasa kwa kusema ukweli dhidi ya
wanachoita uongozi mbaya. Hatua ya kuwafukuza wanachama hao , inasekena ni
kutokana na utovu wa nidhamu.
Wabunge hao walishtakiwa katika kamati ya
nidhamu ya chama na kukabiliwa mashataka saba: kuwapigia debe wagombea wa vyama
vya upinzani katika uchaguzi mdogo; kupaka matope wagombea rasmi wa chama cha
NRM wakati wa uchaguzi mdogo; kutoa madai ya uongo kwa vombo vya habari dhidi
ya chama cha NRM; kutumia majukwaa haramu, kama vile vyombo vya habari na
mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani kuzungumzia masuala
yanayowakera;kujihusisha katika uundaji wa genge ndani mwa NRM; matumizi ya
lugha chafu;na mwisho kukaidi kamati ya nidhamu ya chama.Wote licha ya kuwaita
kufika mbele ya kamati hiyo kujieleza walipinga.
Hii
ndiyo mara ya kwanza tangu mfumo wa vyama vingi kuanza tena mwaka wa 2006,
chama cha NRM kufukuza wanachama wake.
Na
hii imezusha tafsiri tofauti kwa wabunge wanaofukuzwa chama.Katibu mkuu wa NRM
anasema kuwa hii inamaanisha kuwa wamepoteza viti vyao vya ubunge.
Mbabazi
aliongeza kusema kuwa ''Kulingana na sheria za Uganda, hususan kifungu 83 cha
katiba ya taifa ni kuwa mtu anaweza kuwa mbunge pindi tu ikiwa amechaguliwa
kama mbunge wa kujitegemea,au ikiwa amechaguliwa baada ya kuungwa mkono na
chama Fulani,au ni waziri,au kama mwanajeshi.''
Hakuna
njia nyingje ile. Wabunge hao wanasema kuwa katiba haikubali mbunge yeyote
kubadili chama bungeni.Ikiwa mtu atapoteza uungwaji mkono wa chama chake hii
ina maana kuwa amepoteza kiti chake.
Lakini
hilo limepingwa
na mbunge muathiriwa na tena wakili, Wilfred Niwagaba.
Niwagaba
alisema ''Ikiwa anadhani kwa kutusimamisha au kutufukuza uanachama ina maana
kuwa tunapoteza viti vyetu,nasikitika sikubaliani na tafsiri hiyo.Hakuna hata
mmoja wetu ameondoka kutoka chama kwa hiari.''
Hata
hivyo mwenzao Vincent Kyamadidi amesimamishwa uanachama kwa muda kutokana na
madai kuwa alilewa na kujaribu kupigana hadharani jambo ambalo linakwenda
kinyume na maadili ya chama.
Aidha
yeye alipoita kujieleza alifika mbele ya kamati hiyo.
Bado
kuna vuta ni kuvute kuhusu majaliwa ya wabunge wanne, ikisemekana wamekwenda
mahakani kupinga kufukuzwa kwao.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment