Wednesday, April 17, 2013

Camera ya jembe imerudi mtaani....

 Mtu asiyefahamika akiwa amelala kama alivyokutwa na Kamera yetu pembezoni mwa ukuta wa Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam leo.

 Waandishi wa habari wakinunua vitabu mtaa wa Samora karibu na Sanamu la Askari jijini Dar es Salaam leo.

Leo nilipata bahati ya kukutana na watu wengi niliosoma nao, huyu ni dada Caroline Bushiri, nilikuwa naye TSJ, sasa anasoma chuo Kikuu Huria cha Tanzania, na yupo gazeti la chama UHURU kwa mazoezi.

 Anaitwa William Mtutwa, rafiki na mwanafunzi mwenzangu, tulisoma pamoja MOA High School, History, Kiswahili and Literature (HKL) wawili leo tulikutana baada ya miaka 10. Willy ni mwanasheria na jembe ni mwanahabari... Mhhhh

 Abdallah Khamis wa Tanzania Daima akiongeza maarifa, wanahabari tunashauriwa kusoma sana vitabu ili kuwa na ufahamu mkubwa kwenye masuala mengi.

Jumatano ndiyo siku yangu ya kujidai, kwani baada ya kazi nzito ya wiki nzima kuandaa gazeti la Raia Mwema leo ndiyo mzigo umetoka. Naam Raia Mwema linatoka kila Jumatano. Hapa nilikuwa nikijadiliana na rafiki yangu Abdallah, tulikuwa kijiweni MAELEZO mtaa wa Samora Posta jijini Dar es Salaam, nilikuwa nikimweleza umuhimu wa kusoma vitabu, nilimshitua kwa kumwambia nyumbani nina maktaba ndogo ina vitabu 300. Nimemualika amesema atakuja mwisho wa wiki hii...

HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
17 APRIL, 2013

No comments:

Post a Comment