Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
vinywaji baridi ya PEPSI kwa Bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Saad Abdul Latif, hivi karibuni
alifanya ziara nchini Tanzania
ikiwa ni sehemu ya ziara ya kuzitembelea nchi za ukanda wa Afrika Mashariki (Kenya , Tanzania
na Uganda ).
Katika ziara hiyo, Bw. Latif, aliambatana
na Rais wa Kampuni hiyo ya PEPSI kwa bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Sanjeev Chadha, ambapo
waliweza kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo.
“Ni furaha kubwa kuwa hapa nchini Tanzania . Kubwa
ninaomba muwe na uhaikika ya kwamba Kampuni ya PEPSI, imedhamiria kuhakikisha kwamba wateja
wake wanafurahia bidhaa zenye ubora wa kimataifa katika bei nafuu zilizo za
kirafiki,” alisema Bw. Latif.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Bi.
Mapunjo aliishukuru Kampuni hiyo ya PEPSI kutokana na ahadi yake iliyojiwekea ya kusaidia katika suala
zima la maendeleo ya kiuchumi hasa katika juhudi zake za kuboresha viwanda,
masoko, miundombinu na usambazaji.
“Kampuni ya PEPSI nchini (SBC Tanzania ) inazalisha na kutengeneza nafasi za
ajira nchini Tanzania ,”
aliongeza Bi. Mapunjo.
Hivi karibuni Kampuni ya SBC
imeanzisha kiwanda cha kisasa cha PEPSI katika jiji la Nairobi, ambapo matokeo
yake yamekuwa mazuri naya kutia moyo kutoka
kwa wateja. SBC si tu inatoa chaguo la ziada kwa wateja wake kwenye vinywaji
vyake, lakini pia inatoa thamani ya ziada kwa fedha.
Vinywaji hivi vya PEPSI venye ujazo wa
350 ML kwenye glasi kinauzwa bei ya kawaida ambayo ni sawa na bei ya chupa yenye ujazo wa 300 ML. Ni pamoja
na Pepsi, Mirinda, Mountain Dew na aina tofauti za Evervess Kampuni ya SBC Tanzania , ni kampuni pekee inayozalisha bidhaa
mbalimbali za PEPSI nchini Tanzania .
MJENGWA BLOG
No comments:
Post a Comment