Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akimkabidhi picha ya wamasai Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Wanajeshi
22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam . Wanajeshi hao kutoka
chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku
tano.
NA
MAGRETH KINABO
ELIMU ya uzalendo
imesaidia kuwafanya vijana wa Kitanzania kuipenda nchi yao ,
hali iliyochangia nchi yetu kuwa na amani na utulivu.
Kauli hiyo ilitolewa leo na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo,Seth
Kamuhanda wakati akizungumza na ujumbe wa watu 22,baadhi yao ni viongozi
wa utawala na 13 ni wanafunzi wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu wa mafunzo ya
kijeshi kutoka Nigeria.
Ujumbe huo umetembelea wizara
hiyo kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya Utamaduni wa Kitanzania,
umeongozwa na kiongozi wa msafara, Meja Generali, Ati
John,ambaye ni Mkurugenzi wa Jeshi la Wanamaji.
“Mojawapo ya program
tunazowafundisha vijana ili kuondoa migogoro katika
nchi yetu ni elimu ya uzalendo ,yaani tunawafundisha jinsi ya kuipenda
nchi yao .
Elimu hii imesaidia kupunguza migogoro,alisema.” Katibu Mkuu huyo
alipokuwa akijibu swali la mmoja ya wanafunzi hao lililouliza
kuwa kuna program zipi zinazochangia kupunguza migogoro
hususan kwa vijana.
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa
kuna mkakati wa kuwawezesha vijana kiuchumi ili waweze kubuni miradi mbalimbali
kwa kuwa na mfuko wa vijana.
Alisema katika mpango huo
vijana wanakuwa katika vikundi na kufanya shughuli mbalimbali
kuwawezesha kiuchumi.
Aidha Katibu Mkuu huyo
akizungumza kuhusu masuala ya kiutamaduni ,alisema wizara yake ndi yenye
jukumu lakuendeleza Utamaduni wa Mtanzania, hivyo katikawizara hiyo yenye sekta
nne, ambazo ni Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Kamuhanda alisema
sekta ya utamuduni ndio inayofanyakazi ya kudumisha Utamaduni huo.
Aliongeza kuwa lugha ya
Kiswahili ndio imekuwa lugha kuu ya mawasiliano nchini na ndiyo iliyoleta
umoja ,amani na mshikamano.
Wakizungumzia kuhusu
ziara hiyo kiongozi huyo na mmoja wa wanafunzi, Ikema Francis walisema
wameshukuru kwa taarifa walizopata kuhusu wa masuala hayo ya kiutamaduni na
kuhafamu kuwa lugha ya Kiswahili ndiyo imeleta umoja.
No comments:
Post a Comment