Saturday, April 20, 2013

Mwanahabari aacha sherehe ya harusi yake na kushika kazi baada ya tetemeko Uchina.



(Imetokea leo hii) Alikuwa kwenye sherehe yake harusi, baada ya kusikia tetemeko la ardhi, lililoua watu takriban 150 ambalo limeporomosha majengo na barabara kuharibika katika jimbo la Sichuan, kusini Magharibi mwa China msichana huyu aliachana na sherehe na kurudi kazini kupiga mzigo.
 
Hii ni moja ya siri ya Wachina, kuna baadhi ya sehemu HAKUNA msamaha na watu wao wamekubali kupokea hiyo hali na kuigeuza moja ya sehemu ya maisha yao, aah. Ikishasemwa A ni A, basi hapo ni Mei ban fa (hakuna njia mbadala)!

Inadaiwa wanajeshi kama 6000 wamepelekwa kwenda kusaidia katika uokozi zaidi ya kilomita 100 kutoka Chengdu, mji mkuu wa jimbo la Sichuan.

Shughuli za uokozi zinatatanishwa na bara-bara zilizovunjika na simu zilizokatika.
Waziri Mkuu, Li Keqiang, aliwasili huko haraka kuongoza shughuli hizo.

Tetemeko lililotokea katika jimbo la Sichuan mwaka wa 2008 liliuwa watu 90,000.
 Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog.

No comments:

Post a Comment