Friday, April 19, 2013

Leo nimepokea barua nzuri ya pongezi kutoka kwa kaka yangu Ally, si vibaya nanyi mkaisoma. Nasubiri barua zenu pia, kukosoa na kupongeza, lakini napenda sana kukosolewa.


A'alaikum"Sheikh",

Kaka natumaini hujambo na unaendelea vyema na harakati zako.
Ama hakika"nimefurahi" kuona adhma na hadhi yako inakubalika.

Kama ujuavyo si mtu wa kuangalia jambo, kiwepesi na ndiyo hilo limenipa msukumo wa furaha yangu kwako.

Hongera yangu ni kuona tu,tangazo la kibiashara kwenye blog yako kwani ni hatua na dalili njema ya kuwa kazi yako ina muelekeo mzuri na inakubalika.


Daima usikate tamaa kama ujiitavyo jembe basi "Jembe halimtupi Mkulima", jitahidi Ekari bado zimebaki kwani si wote ni wakulima bali wengi wetu ni walaji hivyo soko lipo.Muhimu,boresha kazi,na kwa muda huu jitathmini tangu ulipoanza nini muelekeo wako kujitofautisha na wadau wengine wa habari waBongo.

Tafakari utajua nini uwaletee wa Bongo kwa maana utakata kiu ya habari na kukufungulia soko na kunyanyua kipato chako.


Shukrani,nduguyo
Ally Ahmad

No comments:

Post a Comment