Zaidi ya watu 2,000 mashuhuri duniani wametoa heshima zao
za mwisho kwa hayati Margaret Thatcher katika mkusanyiko mkubwa wa watu tangu
mazishi ya mamake malkia wa Uingereza mwaka 2002.
Jeneza la Bi Thatcher, lilibebwa na kupitishwa katika
barabara za London
likisindikizwa na waombolezaji pamoja na vikosi vitatu vya jeshi la taifa.
Waziri mkuu David Cameron amesma kuwa heshima
hizo zilistahili kwa mtu mashuhuri kama
Thatcher.
Polisi
elfu nne wamshika doria mjini London
, mji ambao umejionea idadi kubwa ya watu waliojitokeza kushuhudia mazishi
hayo.
Kulikuwa
na taarifa za maandamano dhidi ya Thatcher ingawa sio makubwa kama
ilivyotarajiwa.
Mkusanyiko
wa watu katikakanisa la Mtakatifu Paul ulijuimsha familia ya Thatcher pamoja na
waziri wakuu wa zamani ikisemo Tony Blair, Gordon Brown na Sir John Major,
mawaziri wa sasa na wale waliohudumu kama
serikali ya Bi Thatcher.
Majonzi
yalishuhudiwa pamoja na kicheko mara kwa mara huku Askofu wa London , Richard Chartres akiwakumbusha watu
kuhusu Thatcher na kimsifu kwa ukakamavu wake.
Thatcher
alikuwa na ushawishi na mwenye utata na lifariki wiki jana baada ya kuugua
kiharusi
Maelfu
ya watu na maafisa wa kijeshi walipiga foleni katika barabara kuu za mjini London kuusindikiza mwili
wake Bii hatcher.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment