Mechi namba 163 ya Ligi Kuu ya Vodacom
iliyochezwa juzi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Morogoro imeingiza sh. 18,014,000.
Watazamaji 3,145 walikata tiketi kushuhudia
mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,564,252.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,747,898.31.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia
watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,841 na kuingiza sh.
14,205,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000
kilichovutia washabiki 36 na kuingiza sh. 720,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh.
1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 422,877.41.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment