Sunday, April 21, 2013

Soma Barua yaAbsalom Kibanda kuenda kwa Mjengwa.
Wana mabadiliko
Ahsanteni kwa sala zenu, zaidi ahsanteni kwa kuweka mbele utaifa katika masuala mengi ya msingi na kwa kujali kuhoji misingi anuai ya utawala bora.
Ndugu zangu, Kanali Mjengwa kwangu ni mzazi. Nimeguswa na kuugua kwake nikihofia kwamba huenda ameshtushwa na tatizo la mwanae Maggid ambaye kifamilia tuna ujamaa. Baba yangu mdogo ambaye ndiye kipenzi cha baba yangu mzazi Marehemu Mzee Norman Absalom Kibanda Kapyela ameoa dada wa tumbo moja kwa kuzaliwa na Maggid Mjengwa.
Kwa sababu hiyo basi matukio yote haya yanapotokea, kushambuliwa na kujeruhiwa kwangu, kutiwa msukosuko kwa Maggid akiguswa na tukio langu kwa sababu ya ukaribu wake na Ludo na hili la kuugua kwa Kanali Mjengwa yanavuruga na kugusa ndugu na jamaa wengi nikiwapo miye mwenyewe.
Ni kipindi kigumu sana hiki kwangu na kwetu. 

Sent from my iPad
CHANZO: Mabadiliko Forum

No comments:

Post a Comment