NA: ONESMO NGOWI
Shirikishoi la Ngumi la Kimataifa (IBF)
limeteua mwamuzi na majaji wa pambano la kutetea ubingwa wa Afrika kati ya
anayeushukilia ubingwa huo Francis Cheka wa Tanzania na mpinzani wake Thomas
Mashali ambaye ni bingwa wa uzito wa Middle ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
(ECAPBA).
Mwamuzi wa mpambano huo wa kukata na shoka atakuwa ni John Shipanuka kutoka
nchini Zambia
mbaye alilisimamia pambano kati ya Francis Cheka na Mada Maugo mwaka jana kwa
ustadi mkubwa. Shipanuka ni Afisa Ugavi katika jeshi la Jamhuri ya Watu wa Zambia na
ana ujuzi mkubwa wa kusimamia mapambano ya ngumi ya kimataifa.
Aidha, majaji wa mpambano huo ni Daudi
Chikwanje kutoka Malawi
ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi Cha Malawi na ambaye anakuwa jaji namba
moja. Steve Okumu wa Kenya
ambaye anakuwa jaji namba mbili na Ismail Sekisambu wa Uganda ambaye
anakuwa jaji namba tatu. Msimamizi mkuu wa mpambano huo ni Rais wa IBF
katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo
Ngowi.
Hata hivyo Ngowi amemwagiza
Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango na Ushindi wa Kamisheni ya Ngumi za
Kulipwa Nchini (TPBC) Boniface Wambura amshikie nafasi hiyo ili Ngowi apate
nafasi nzuri ya kusimamia mapambano matatu ambayo ni (la ubingwa wa Dunia kwa
vijana,, lingine la ubingwa wa mabara kwa wanawake na lingine ubingwa wa
Afrika) yatakayofanyika nchini Ghana tarehe 3 mwezi Mei.
Nayo Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa
nchini TPBC imeshateua maofisa watakaosimamia mapambano ya awali pamoja na
kutoa kibali kwa kampuni ya Mumask Investment and Gebby ili iendeshe mpambano
huo!
Hii ni mara ya pili kwa bondia
Francis Cheka kutetea ubingwa wake tangu amsambaratishe kwa TKO bondia
machachari Mada Maugo katika mpambano uliofanyika mwaka jana mwezi wa Aprili
katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es
Salaam .
<
No comments:
Post a Comment