Monday, April 22, 2013

Wanahabari leo walinolewa katika semina na kuujua mchezo wa Badminton katika klabu ya mchezo huo Khalsa Sports Club, Kisutu jijini Dar es Salaam.

 Katibu wa mchezo wa Badminton Tanzania Dk Wilberd Kente akiwapa somo wanahabari namna ya kucheza mchezo huo, leo.

 Wanahabari wakisikiliza kwa makini maelezo ya Dk. Kente namna ya kucheza mchezo wa Badminton.

 Sheria za mchezo wa Badminton hazitofautiani sana na mchezo wa volleyball tofauti ni kuwa Badminton unachezwa kwa vifaa lakini valleyball unachekwa kwa mikono mitupu huku waitumia mpira.

 Wachezaji Badminton wakicheza mchezo huo kwa style ya Doubles, ambayo hushirikisha wachezaji wanne, wawili kila upande. Lakini kuna mchezo wa Singles, ambao hushirikisha wachezaji wawili mmoja kila upande.

 Dada pekee ambaye jina lake hatukufanikiwa kulipata akishiriki mazoezi ya mchezo huo ambao hauna umaarufu sana Tanzania.

 Katibu mwenezi wa mchezo huo nchini Mzee Timothy Kahoho ambaye pia ni mwanahabari kitaaluma akielekeza jambo wakati wa semina hiyo leo jioni.

 Katibu msaidizi wa mchezo huo Tanzania Tony Desouza (mwenye fulana nyeupe) akielekeza jambo kwa wachezaji wakati wa semina.

 Dk Kente akimwelekeza mmoja wa wanahabari waliohudhuria semina hiyo namna ya kucheza mchezo wa Badminton.

Mwenyekiti wa Badminton Tanzania Arun Jobanputra (mwenye miwani) akimuelekeza namna ya kushika kifaa cha luchezea mchezo huo mwanahabari Anfrey Shayo wakati wa semina leo.

Mchezo wa Badminton umekosa umaarufu nchini kutokana na mwamko mdogo kutoka kwa watu wanaopenda michezo.

kwa mujibu wa katibu wa mchezo huo Dk Wilberd Kente, mchezo wa Badminton umeweza kutoa vipaji vikubwa miaka ya nyuma tofauti na sasa. Kwa kuona umuhimu wa kuurudisha mchezo huo klabu ya Badminton jijini Dar es Salaam wameamua kuanzisha mashindano yatakayoanza Aprili 26 mpaka Mei 1 sikuu ya wafanyakazi.

washindi watapata vikombe na kuhakikisha wanatafuta viwanja maalum vya mchezo huo kwani Dk. Kente alisikitika kuwa shule za Azania, Tambaza na Kisutu zilikuwa na kumbi kwa ajili ya kuchez amchezo huo lakini kumbi zimekuwa zikitumika kwa sherehe za harusi hivyuo kukosa nafasi.

michezo hiyo ya siku tano itaanza saa nne asubuhi mpaka saa 12 jioni katika ukumbi wa Anadil Burhan na Khalsa Sports Club Kisutu jijini Dar es Salaam.

HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
22 April, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA


No comments:

Post a Comment