MBUNGE wa jimbo la Arusha mjini Godbless lema ameachiwa huru kwa
dhamana na mahakama ya hakimu mkazi baada ya kusota rumande kwenye kituo kikuu
cha polisi kwa siku tatu kwa kosa la kuchochea vurugu chuoni uhasibu huku
baada ya kutoka akiwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kumzomea mkuu wa
mkoa.
Lema alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa Tatu na robo
asubuhi akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kufikishwa mbele ya hakimu Devotha
Msele na ndipo mwendesha mashtaka Eliang’enyi Njiro alisimama kuanza
kumsomewa mashtaka ya uchochezi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani
aliyoyafanya kwenye eneo la chuo cha uhasibu njiro jijini Arusha.
Baada ya kutoka mahakamani hapo alielekea kwenye ofisi za chama
hicho na kuzungumza na waandishi wa habari huku akitoa malalamiko na kuwataka
wanachama na wapenzi wa chadema kumzomea mkuu wa mkoa iwe kanisani,mskitini,au
kwenye sherehe mbali mbali,
“Nawatakeni kumzomea huyo mkuu wa mkoa Magessa Mulongo na kuwa nia
ya kumshtaki ipo pale pale ndugu zangu Makamanda wenzangu huyu jamaa awe
msikitini kanisani kote tumzome hiyo itakuwa ndiyo salamu yetu kwake”alisema
Lema
Katika hali nyingine jeshi la polisi liliimarisha ulinzi tangu nje
ya mahakama hadi ndani ya mahakama hiyo kiasi utulivu katika mahakama hiyo
ulionekana na shughuli kuendelea bila bughaa.
Hali kwenye mitaa mbali mbali ya viunga vya jiji la Arusha
ilionekana kuendelea na mishughuliko ya kila siku kama
kawaida kuliko ilivyokuwa ikionekana huko mwanzo kwenye kesi zilizokuwa
zikimkabili mbunge huyo kwa wakazi wa jiji hili kuacha shughuli zao na kuelekea
mahakamani kufuatilia kesi ya mbunge huyo.
Chanzo: Mahmoud Ahmad
No comments:
Post a Comment