Thursday, April 18, 2013

Mazishi ya Bi Kidude katika picha jana na leo.

 Mwili wa Marehemu Bi Kidude ukiwasili nyumbani kwake Raha Leo, ukitokea kwa jamaa zake alipofariki jana kijiji cha Kihinani mjini Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein (katikati) akitoa salamu za mwisho kwa marehemu Bi Kidude nyumbani kwake Raha Leo kabla ya maziko.

 Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba (wa kwanza kushoto) ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Bi Kidude akiwa katika mazishi leo.

 Nassib au Diamond, mwanamuziki wa kizazi kipya (Mwenye kizibao) akiwa kwenye ibada ya kumuombea Bi Kidude leo. Wengine katika picha ni viongozi wa juu wa Serikali ya Zanzibar wa pili baada ya Diamond ni Waziri wa Afya wa baraza la Mapinduzi Juma Duni Hajji, kwa mbaali anaonekana Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Sheif Sharrif Hamad.

 Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein na makamu wa Rais Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal wakiongoza mamia ya waumini wa dini ya kiislam kwenye sala ya kumuombe a Bi Kidude katika msikiti wa Mwembeshauri, kabla ya kupelekwa makaburini katika kijiji cha Kitumba Zanzibar.

Hapa ni nyumbani kwa Bi Kidude eneo la Raha Leo nyuma ya kituo cha Radio saut ya Zanzibar. Vijana wakiandaa tanga.

Picha kwa hisani ya mtandao.

No comments:

Post a Comment