Tuesday, April 16, 2013

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad anazuru nchi tatu za Afrika katika ziara yake ya mwisho ya kigeni kabla ya kuondoka mamlakani baada ya kutawala mihula miwili.



Hata hivyo haijashangaza sana kuwa amemua kuzuru Afrika. Wakati wa miaka minane ya utawala wake, amejikakamua kushirikiana na nchi nyingi za kiafrika na zile za Amerika ya Kusini ambazo nchi hiyo ina uhusiano wa kidiplomasia nazo.
Kuimarisha uhusiano na nchi zinazostawi imekuwa kipaombele kwa Iran na mkutano wa kwanza wa Rais Ahamdinejad umekuwa na rais wa Mali siku kadhaa baada ya kushinda uchaguzi mwaka 2005.
Wadadisi wanasema kuwa kuna sababu za kutosha za kidiplomasia, kwa sera hii ya bwana Ahmadinejad.
Huku shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa zikiendelea kuongezeka na athari zaidi za vikwazo vya kiuchumi, Iran ilihitaji washirika kuunga mkono nchini hiyo kwakatika baraza la Umoja wa Mataifa.
Lengo lake halikutumia kwa sababu ya nchi nyingi zinazostawi kutegemea msaada kutoka kwa Marekani na mashirika mengine ya kimataifa ambayo yana ushawishi wa Marekani na washirika wake.
Kutaka nchi maskini kujizuia kupiga kura katika umoja wa mataifa kuhusu Iran, ndilo jambo pekee ambalo angependa lifanyike.
Lengo kuu la mapinduzi ya kiisilamu mwaka 1979 ilikuwa ni kueneza harakati za uisilamu kote duniani.

Afrika, ikiwa na nchi za kiisilamu si haba, ikawa ya kwanza kuonekana kana kwamba inaweza kuunga mkono Iran.
Mahmoud Ahmadineja Alikuwa rais wa kwanza wa Iran mwaka 2005
      Mnamo Oktoba 2005, aliona uwezekano wa kuondoa Israel na pahala pake kuwa taifa huru la                               Palestina.
      Matamshi yake yalitafsiriwa kama uchochezi wa kutaka kuiondoa Israel kwenye ramani ya dunia.
      Anasifika kwa kuishi maisha ya kiwango cha kadri na amekuwa akipinga ufisadi
      Inaarifiwa hakutumia pesa zozote katika kampeini yake ya urais
Mnamo mwaka 2009 alirejea mamlakani huku maandamano yakifanywa kupinga kuchaguliwa kwake na yakawa mabaya zaidi kushuhudiwa nchini humo tangu mwaka 1979
Sheikh Zakzaky, kiongozi wa waisilamu wa Shia nchini Nigeria,alikuwa mmoja wa waliopigia debe sana madhehebu ya Shia wakati wa mapinduzi nchini Iran.
Ingawa bwana Zakzaky anakanusha kuwahi kupokea msaada kutoka kwa Iran, mhubiri huyu anayepinga vikali Marekani, ana picha ya kiongozi mapinduzi ya Iran Ayatollah Khomeini nyumbani kwake.
Mwaka 2008, rais Ahmadinejad alimpokea aliyekuwa rais wa Comoros wakati huo, Ahmed Abdallah Mohamed Sambi mjini Tehran.
Mhubiri wa madhehebu ya Sunni, bwana Sambi alisomea dini nchini Iran na alikuwa mwanafunzi wa Ahmadinejad.
Wakati wa utawala wa Ahmadinejad, aliimarisha Uhusiano wa kibiashara na kiuchumi. Mapema mwaka huu, Iran ilisema kuwa biashara kati ya Iran na nchi zingine ambazo zimefika thamani ya dola bilioni moja.
Mfano mmoja ni uwekezaji wa Iran barani Afrika ulioanza mwaka 2007 kwa kufungua kiwanda kikubwa cha magari nchini Senegal.

Kutengeza Silaha?

Hata hivyo, Iran ina malengo mengine katika kushirikiana na Afrika. Kuna ripoti kuwa kwa kutumia biashara, Iran inajaribu kukiuka sheria ya vikwazo vya kimataifa.
Zaidi ya miaka miwili iliyopita, Nigeria iliripoti kunaswa kwa silaha zilizokuwa zinatoka Iran,ikisemekana kuwa zilikuwa zinaelekea nchini Gambia.
Mwezi mmoja baadaye bila kuelezea sababu zozote, Gambia ilikata uhusiano na Iran.
Mwaka jana serikali ya Sudan,iliituhumu Israel kwa kushambulia kiwanda chake cha silaha. Israel hata hivyo haikukubali au kukanusha kuhusika na shambulio hilo dhidi ya kiwanda cha Sudan kilichoaminika kupeleka silaha katika Ukanda wa Gaza. .
Iran haijawahi kuzungumzia tukio hilo.
Licha ya Iran kuwa na uhushiano na nchi nyingi zinazostawi, wadadisi wanasema kuwa haijaathiri kivyovyote ushawishi wa Marekani kwa nchi hizo.
Chanzo: BBC Swahili.







lvetica� h

No comments:

Post a Comment