Saturday, April 20, 2013

Wanahabari wapewa semina kuhusu mashine za kulipa kodi Tanzania.

 Mkurugenzi wa huduma za kodi na elimu mamlaka ya mapato Tanzania Richard Kayombo akizungumza na wanahabar katika Hoteli ya Court Yard leo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kuhusu mfumo wa malipo kwa kutumia mashine za elektroniki ulioanza mwaka 2010.

 Jopo la wakurugenzi wa idara ya huduma na elimu mamlaka ya mapato Tanzania walikisikiliza wachangiaji katika semina hiyo leo kutoka kulia ni dada Alvera Ndabagoge afisa elimu mwandamizi idara ya kazi za ndani, wa pili kutoka kulia ni meneja huduma mamlaka ya mapato Tanzania Aleru kiula, wa tatu ni mkurugenzi wa huduma na elimu Richard Kayombo, wa nne ni dada Dyana Masala meneja wa elimu, wa nne ni Hamis Lupeja afisa mwandamizi mkuu wa elimu na huduma.

 Richard Kayombo akifurahia jambo wakati semina ikiendelea, semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na mamlaka ya Mapato Tanzania imelenga kuwapa elimu wanahabari kuhusiana na matumizi ya mashine za elektroniki katika kulipa kodi. Pia semina hiyo ililenga kutoa elimu kwa wananchi namna ya umuhimu wa kudai risiti wakati wa manunuzi. Wanahabari wametumika kufikisha ujumbe kwa wananchi.

 Washiriki wa semina hiyo wakichangia mada wakati wa maswali na majibu kwenye hoteli ya Court Yard jijini leo.

 Mkurugenzi wa idara ya huduma na elimu mamlaka ya mapato Tanzania Richard kayombo akibadilishana mawazo na wanahabari wakati wa mapumziko.

Mtoa mada wa leo ambaye ni Ofisa mwandamizi mkuu wa idara ya elimu na huduma za kidi malaka ya mapato tanzania Hamisi Lupeja akiwasilisha mada yake leo mbele ya wanahabari.

No comments:

Post a Comment