Ligi kuu ya soka nchini England itaendelea tena jumatatu ya leo kwa
mchezo mmoja kati ya Manchester
United watakaokuwa nyumbani kwenye uwanja wa Old Traford kuwakaribisha Aston
Villa.
Mchezo
huo ambao Manchester United inahitaji ipate
ushindi kujihakikisha ubingwa wa 20 wa ligi kuu soka nchini England na kuweka rekodi mpya ya kuwa timu
iliyochukua taji hilo mara nyingi zaidi ya Liverpool ambayo ilikuwa inashikilia rekodi ya mataji 19.
United
inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa imetoka kulazimishwa sare ya 2-2 na West Ham
United katika mchezo wa jumatano iliyopita. Aston Villa wao watashuka uwanjani
kucheza mchezo huo usiku wa leo wakiwa kwenye harakati za kuepuka kushuka
daraja la ligi kuu.
United
katika michezo mitano iliyopita waliyocheza wamefungwa michezo
miwili,wameshinda miwili na kutoka sare mmoja huku Aston Villa katika michezo
mitano iliyopita waliyocheza wamefungwa mchezo mmoja na kushinda michezo mitatu
na kutoka sare moja dhidi ya Fulham.
Huu
utakuwa mchezo wa 34 kwa timu zote kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza msimu
huu ambapo zitakuwa zimebakisha michezo mingine minne kumaliza ligi.
United wanaongoza ligi wakiwa na point 81 huku
wakifuatiwa na watani zao wa wajadi Manchester City ambao walifungwa hapo jana
jumapili na Tottenham kwa mabao 3-1,hivyo mchezo wa leo utaweza kuwafanya
United wacheze kwa uhuru zaidi na kutaka kujipa matumaini ya kuwavua rasmi
ubingwa majirani zao Manchester City. Aston Villa inayofundishwa na Paul
Lambert inashika nafasi ya 17 wakiwa na point 34,pointi tatu zaidi ya Wigan wenye pointi 31 wakiwa kwenye nafasi ya 18 ambayo
ni kwenye kundi la timu tatu za mwisho zilizoko kwenye hatihati ya kushuka
daraja.
Aston
Villa katika michezo 32 iliyopita waliyocheza na Manchester United wameshinda
mchezo mmoja,hiyo ilikuwa mwaka 2009 mwezi disemba pale Gabby Agbonlahor
alipofunga bao la kichwa kwenye uwanja wa Old Traford. Kwa upande wa United,
wao katika michezo 34 iliyopita ya ligi kuu tangu mwaka 1995 wamepoteza mara
moja tu dhidi ya Villa.
Wayne
Rooney anatarajia kufikisha mchezo wake wa 400 akiwa na Manchester
United huku akiwa ameifungia klabu yake mabao tisa ya ligi kuu dhidi ya Aston
Villa ikiwa ni rekodi nzuri kwake kuifunga timu moja idadi kubwa ya
magoli,akiwa amezifunga idadi hiyo hivyo timu za Bolton, Fulham and Newcastle .
Manchester United itataka kuvunja rekodi ya Chelsea ya msimu wa
2004/05 kwa kumaliza msimu na idadi kubwa ya pointi, iwapo watashinda mechi
zote zilizosalia,huenda wataifikia rekodi ya pointi 95 za Chelsea .
Mshambuliaji
wa Aston Villa Christian Benteke yupo kwenye kiwango kizuri hivi sasa baada ya
kufunga mabao 10 katika mechi 13 zilizopita alizoichezea Villa huku akiwa
amebakisha magoli mawili ili afikie rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa timu
hiyo Dwight Yorke ya kufunga magoli mengi(17)katika msimu mmoja wa ligi kuu,ila
ndiye mchezaji ambaye anaongoza kwa kuotea mipira mingi(offsides) kwenye ligi
kuu msimu huu, ambapo amekwisha otea mara 49.
Mwenzake
Gabby Agbonlahor yeye amebakisha goli moja ili aweze kuvunja rekodi ya
mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa, Dwight Yorke ya kufunga magoli mengi
kwenye klabu hiyo. Yorke anaongoza kwa kufunga magoli 60 kwenye timu ya Aston
Villa.
Nyota
wa zamani wa Aston Villa ambaye kwa sasa anaichezea Manchester United Ashley
Young ataikosa mechi hiyo dhidi ya timu yake ya zamani kutokana kuwa majeruhi.
Mchezo huu utakuwa ni mtihani mwingine kwa mshambuliaji wa Manchester United,
Robin Van Persie ambaye anasaka kiatu cha ufungaji bora wa ligi kuu kwa mara ya
pili mfululizo. Hivi sasa Van Persie ana magoli 21 akiwa anashika nafasi ya pili
nyuma ya Luis Suarez wa Liverpool ambaye ana
magoli 23 akiongoza safu ya wafungaji kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Mchezo
huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa nne za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment