Sunday, April 28, 2013

Wanaume wengi huvutiwa kufanya mapenzi na wake wa rafiki zao...



Tafiti nyingi duniani zimegundua kuwapo na msukumo na mhemko wa tamaa za ngono kwa wanaume. Majibu kadha wa kadha ya tafiti hizo yamekuwa yakitoa majibu sawa, ikiwemo suala la maumbile ya mwanamume na namna anavyompokea mwanamke yoyote machoni pake.

“Rafiki yangu wa karibu niliyempokea na kumtafutia kazi nchini Marekani alinisaliti kwa kutembea na mume wangu,” anaanza kwa kusema Christina Edward (34) (siyo jina lake kamili) Mtanzania anayeishi katika Jimbo la Houston Texas nchini Marekani.

Christina anasema haikumuwia rahisi kung’amua tukio hilo la aibu, mpaka alipotonywa na jirani yake ambaye hakuwa na ukaribu naye. “Jirani yangu aliwaona, akanipa taarifa za usaliti huo. Nilifuatilia kwa muda mrefu na kuwakuta wakiwa katika flat (nyumba) anayoishi rafiki yangu huyo iliniuma sana, mpaka leo siwezi sahau tukio lile japo miezi kadhaa imepita sasa nahisi aibu kila wakati,” Huyu ni mmoja kati ya mamilioni ya wanawake duniani wanaokumbana na adha za namna hii. Mwananchi liliwafanyia mahojiano baadhi ya wanasaikolojia ambao walithibitisha kuwapo na ukubwa wa tatizo hilo hapa nchini, wakilinganisha kesi wanazozipokea zinazohusiana na usaliti wa waume na wake waliopo ndani ya ndoa.

Kauli ya wataalamu
wa saikolojia
Mwanasaikolojia na Mkurugenzi wa Kliniki ya NEHOTA inayotoa huduma ya ushauri iliyopo Makongo Juu jijini, Dk Bonaventura Balige anasema japo tafiti kadhaa zimefanyika, lakini Tanzania hakuna utafiti uliofanyika mpaka sasa, ila anakubaliana na tafiti za nje kulingana na kesi anazozipokea na uzoefu wake katika maisha ya kawaida.

“Nakubaliana na tafiti zilizowahi kufanyika nje, kituo changu kimepokea kesi kadhaa kama hizo na zifananazo na hizo. Mara nyingi tunapopokea kesi huwashauri kwanza kutafuta chanzo cha tatizo. Stress (msongo wa mawazo) ndiyo huwa chanzo cha wanaume walio wengi kujikuta wakiingia katika vitendo hivyo.”

Anasema msongo wa mawazo kwa wanaume husababishwa na vitu vingi, ikiwamo kazini, mtaani au nyumbani kwake, mwanamke asipokuwa makini hujikuta familia yake ikiwa mashakani.

Dk Balige anasema amepokea kesi zaidi ya tatu zilizohusu mume kuwa na uhusiano ya kimapenzi na rafiki wa mkewe, lakini pia amepokea kesi zaidi ya nne za waume kutembea na wafanyakazi wa ndani wa kike wake zao wakiwa kazini.
Hata hivyo amewahi kupokea kesi kadhaa za wake kutembea na rafiki za waume zao. huku lukuki zikiwa ni usaliti katika ndoa.
“Licha ya kuumbwa hivyo mwanamume huyu ana uwezo wa kupenda mwanamke mmoja tu, ila kinachomfanya awe na wanawake wengi ni tamaa.
Wapo wanaoweza kudhibiti tamaa zao, lakini wengine ni vigumu. Dk Balige anasema kuwa mwanamume akishindwa kuhimili mhemko wa mwili wake, huwa chanzo cha kuharibu uchumi wa familia na mwishowe huishia kutelekeza familia “wanawake nao wanatumia udhaifu wa wanaume katika kuchuma pesa, hivyo mwanamume asipoweza kuzisimamia hisia zake hujikuta akitelekeza familia,” anasema.

Mwanasaikolojia Jaykesh Rathid mwenye asili ya Asia aliyefungua ofisi inayotoa huduma ya ushauri maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam anasema, wanaume wana kawaida ya kutongoza wanawake waliowazoea wakiwamo rafiki za wake zao kwa kuwa huwawia rahisi wakati wa kujieleza. “Mara chache sana mwanamume kutongoza mwanamke anayekutana naye kwa mara ya kwanza.
Waume wengi hawana kawaida hiyo hasa waliooa, kwanza hufikiria mtu anayetongoza hamfahamu kiundani huenda anaweza kuwa ndugu au mtu wa karibu na mkewe, huona afadhali kwa mtu anayemjua au anayefanya naye kazi ofisi moja,” anasema Jaykesh. Jaykesh anasema kiashiria huwa sababu ya kwanza kwa mtu kufanya kitendo hicho “kabla rafiki wa mke hajafanya kosa hilo, mara nyingi mwanamume au yeye mwanamke huonyesha ishara ya kumpenda mhusika, na kwa kuwa anafahamu baadhi ya mambo kupitia kwa mkewe, humwia rahisi kujua mbinu zipi atumie kumpata,” anasema.

Anasema mwanamume ameumbwa na tamaa “Hii isipothibitiwa na mke mwanamume atatoka nje, kesi nyingi napokea hapa ni watu wa karibu, inaweza kuwa rafiki wa mke, msichana wa kazi za ndani au mtu anayefanya naye ofisini au maeneo mengine ya kazi.”

Kisa na mkasa halisi
kilichowahi kutokea
Kisa cha Christina, Mtanzania aliyeolewa na raia wa Marekani kilitokana na kumpa uhuru rafiki yake aliyemwamini kuwa anaweza kuwa mlinzi mzuri katika nyumba yake kwa kipindi anachotafuta kazi, huku yeye akifanya kazi shifti ya usiku.

“Nilimlipia nauli ya ndege kutoka Tanzania baada ya miezi mitatu alifanikiwa kupata chuo na kazi. Mbadala wake alihama harakaharaka. Mawasiliano yalikuwa ya mbali mpaka nilipopata taarifa kuwa ananichukulia mume.”

Edina aliyekataa kutaja jina lake la pili anasema alizoeana na mpangaji mwenzake kwa muda mrefu na kuwa marafiki. Baadaye aligundua alikuwa na uhusiano na mumewe.

“Nilimwona kama msiri wangu alikuwa akinieleza habari zake nami nilimweleza zangu kwa kuwa wote tuliishi na waume. Lakini mumewe akisafiri alikuwa akiondoka mida ya jioni na mume wangu alichelewa kurudi nyumbani. Baadaye niligundua kuwa ananichukulia mume baada ya kuzikuta meseji za mapenzi kwenye simu ya mume wangu.”
Munira anasema aliolewa kwa ndoa ya kikristo. Lakini ndoa hiyo iliingia shubiri baada ya msimamizi wa ndoa yao kuanza kutoka na mumewe “Kesi ilikuwa nzito japokuwa hatukufanikiwa kupata ushahidi, lakini tuliwafumania wakiwa hotelini pamoja wakipata chakula cha usiku. Kesi hii ilinguruma kwa muda mrefu mpaka tulipowaona washauri ndipo tatizo hili liliisha.Binti mwingine anasimulia kisa kilichomkuta miaka miwili iliyopita baada ya kuachana na rafiki yake wa kiume (boyfriend) baada ya uhusiano wao kuingiliwa na rafiki yake wa karibu.

Hata hivyo, Salum mkazi wa Tabata Segerea jijini Dar es Salaam yeye anasema mkewe aliwahi kumfumania akiwa na mwanamke mwingine “Mke wangu alinifumania nikiwa na mwanamke mwingine niliyemfahamu kupitia yeye japo hawakuwa marafiki, alinisamehe, lakini katu sidhani kama ninaweza kuvumilia nikimfumania mke wangu,” anasema Salum.

Tafiti nyingine
Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani mwaka huu umebaini kuwa wanaume huwa na mawazo ya kufanya ngono na marafiki wa wake zao, huku baadhi yao wakifanikiwa kutimiza ndoto zao.

Chuo Kikuu cha Utafiti cha Missouri kimegundua kwamba wanaume huwaweka wake zao kundi moja na rafiki zao, hivyo hupelekea kumtamani huku baadhi yao wakiridhishana kimapenzi. Mawazo hayo hupelekea kuanza kuonyesha viashiria vya mapenzi ambapo mwanamume hujitahidi kuwa na ukaribu zaidi na mtu huyo.

“Ingawaje wanaume wengi wana nafasi kubwa ya kufanya ngono na rafiki za wake zao, uwezekano wa maazimio ya jambo hilo ni mdogo,” anasema kiongozi wa utafiti huo, profesa Mark Flinn.
MWANANCHI
a� �

No comments:

Post a Comment