Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anatarajiwa kupandishwa
kizimbani kujibu mashtaka ya uchochezi na kusababisha vurugu kwenye chuo cha
uhasibu mwanzoni mwa wiki hii jijini hapa mbali na lema teyari jeshi la polisi
limewapandisha kizimbani watu 14 kwa kuthuma kama hizo.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa
polisi(ACP) Liberatus Sabas alisema kuwa mh.lema atapandishwa kizimbani kujibu
tuhuma hizo kwenye mahakama ya wilaya siku ya jumatatu mkoani hapa.
Kamanda Sabas alisema kuwa jeshi hilo lilifanikiwa kumtia nguvuni
lema huko nyumbani kwake Njiro majira ya 9 usiku wa kuamkia jana na anaendelea
na mahojiano na jeshi hilo na kuwa atafikishwa mahakamani siku hiyo.
Vurugu hizo zilitokea juzi baada ya mwanafunzi mmoja Hendry Kagu
22 kuuwawa kwa kuchomwa na kisu na watu wasiojulikana na kupoteza maisha ndipo
wanafunzi hao walianza kujikusanya kwa madai ya kujadili kifo cha mwanzao na
ndipo mbunge huyo alifika na kuanza kuwashawishi kwenda ofisini kwa mkuu wa
mkoa kwa maandamano lakini kabla ya kuanza maandamano hayo mkuu wa mkoa Magessa
Mulongo alifika eneo la chuo cha uhasibu kusikiliza tatizo hilo.
Hali ya tafrani na kuzomea ilitawala eneo hilo ndipo baada ya
Mulongo kufika hali iliyoleta sintofahamu hadi rc Mulongo kundoka na ndipo
askari wa kikosi cha kutuliza fujo walipoamua kuwatawanya kwa mabomu ya machozi
na hali kutulia na kisha mkuu wa mkoa kuamuru chuo hicho kufungwa kwa muda
usiojulikana hali iliyoleta simanzi kwa wanafunzi ambao walikuwa wakijianda
kufanya mitihani yao ya kumaliza chuoni hapo wiki inayokuja.
No comments:
Post a Comment