Wednesday, April 17, 2013

Bi Kidude hatunaye.... Nguzo ya pili ya Taarab yaanguka baada ya nguzo ya kwanza kuanguka siku moja iliyopita wote kutoka Zanzibar.

Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa mwanamuziki mkongwe wa sanaa ya Taarab na Unyago Bi Fatma Baraka maarufu Bi kidude amefariki dunia.

Bi Kidude ambaye alinza muziki mwaka 1920, tarehe yake ya kuzaliwa haijulikani kwani hata yeye alishindwa kujibu kitendawili hicho enzi za uhai wake, ila itabaki tu kuwa Bibi huo anayeshikilia tuzo ya Womex aliyoipata mwaka 2005 ambayo ni mwanamke mwenye mafanikio zaidi katika Taarab na nyimbo za unyago ni mwanamuziki mwenye umri mkubwa kwa Afrika.

Taarifa zaidi zitawajia baadaye baada ya kluwasiliana na ndugu wa familia, Itakumbukwa Bi kidude alizushiwa kifo kwa muda mrefu ila siku ya leo ahadi yake imetimia.
HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
17 April, 2013
Dar es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment