Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe azungumzia suala la kutishiwa kwa silaha mama yake mzazi.
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa
na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba
"Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu
mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi
hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.
Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi.
Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni
mama wa kawaida wa kitanzania kama mama
mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa
kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote
ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka
zitachukuliwa.
Ushauri- tuwe makini na "Agente
provocatuers" au in English "provocation agents" nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against
provocations. Nadhani mmenipata"
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa
Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi,
umasikini na ugandamizaji.
Chanzo: Facebook
No comments:
Post a Comment