Thursday, April 18, 2013

Tamko la TCRA kuhusu kusajili kadi za simu.

 Mkurugenzi wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof JOHN NKOMA  mapema leo asubuhi akitoa tamko juu ya usajili wa namba za simu za mkononi.
 Mkurugenzi wa Vodacom RENE MEZA, naye alikuwepo katika tamko hilo.

 Mkurugenzi wa Zantel PRATAP GHOSE, pia alishiriki tamko hilo la pamoja.

Mkurugenzi wa Airtel SUNIL CALASO, pia alikuwepo na nikashangaa kwanini wakurugenzi wote wa mitandao ya simu ni wahindi?


Mkurugenzi wa  mamlaka ya mawasiliano nchini John Nkoma,ametoa tamko la pamoja lililoazimiwa kwa kushirikiana na makampuni ya simu kuwa watumiaji wote wa simu za mkononi ambao hawajasajili namba zao wafanye hivyo mara moja, kwani utaratibu unaofuata ni kufunga namba zote ambazo hazijasajiliwa.


Akifafanua zaidi juu ya msimamo huo Nkoma alisema ni kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano au kifungo cha miezi mitatu jela.

Aidha amewataka  wananchi kuhakiki usajili wao kwa kupiga nyota 106 alama ya reli, ili kujua kama wamesajiliwa.  utapata ujumbe wa taarifa zako za usajili,na kama taarifa si sahihi tafadhali wasiliana na kampuni husuka haraka sana.

Mjengwa.com

No comments:

Post a Comment