Katika kijiji kimoja Kaskazini mwa Tanzania , ndege aina ya Boeing 747 zinatua
kwenye kiwanja binafsi, magari yenye nambari za usajili za milki za kiarabu,
zikiendeshwa katika eneo hilo
na yeyote mwenye simu ya mkononi anapotua hapo hupokea ujumbe ambao haukutarajiwa:
''Hujambo mgeni na karibu UAE.''
Kwa karne nyingi, (Savanna) katika eneo la
Arusha lilikuwa makao kwa watu wa jamii ya wamaasai lakini siku hizi mtu sasa
anaweza kudhania yuko Dubai
moja ya nchi za milki za kiarabu.
Hii
ni kwa sababu sehemu kubwa ya ardhi mjini Arusha hasa katika eneo la Loliondo
karibu na mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Serengeti imekodishwa kwa kampuni ya
uwindaji ya Emirati iitwayo Ortello
Tangu
mwaka 1992, kampuni hiyo imekuwa ikiwapeleka kwa ndege watalii matajiri zaidi
kuwinda simba na wanyama wengine hali iliyowaghadhabisha wenyeji wa eneo hilo ambao ni wamaasai
ambao wamezuiwa kuwalisha mifugo wao katika maeneo ya kuwinda.
Sasa
serikali ya Tanzania
inataka kutoa ardhi zaidi kwa wawindaji hao kwa lengo la kujenga barabara ya
umbali wa kilomita 1,500 ambako wanyamapori watakuwa wakipita kwa manufaa ya
kampuni hiyo ya uwandaji.
Mpango
huo utawaathiri takriban watu 30,000 watakaoachwa bila makao na pia kuwaathiri
maelfu ya wengine, ambao huwalisha mifugo wao katika maeneo hayo wakati wa
msimu wa kiangazi.
Wamaasai
wameghadhabishwa mno na hata kufanya maandamano, wakisema kuwa maisha yao yataathirika pakubwa.
Zaidi
ya asilimia ya 90 ya wakaazi wa Loliondo ni wa Maasai ambao hutegemea kuwalisha
mifugo wao nyasi kutoka eneo ambalo serikali inanuia kuwakodishia waarabu.
"bila
Ardhi hatuwezi kuishi,'' anasema mama Naishirita Tenemeri, mwenye watoto
watatu.
Bi
Tenemeri anafuga Ng'ombe na Mbuzi eneo la Loliondo, ili kuwanunulia chakula na
kuwalipia karo ya shule wanawe.
Wa Maasai wana historia ya kupoteza ardhi yao
nchini Tanzania
tangu wazungu walipowahamisha kutoka mbuga ya Serengeti mwaka 1959.
Mapema
mwezi huu, Bi Tenemeri, akiwa amejifunga shuka yake nyekundu, alijiunga na watu
1,000 wengi wao wakiwa wanawake chini ya miti ya mivule, katika kijiji cha
Olorien kupinga mipango ya serikali kuuza ardhi yao .
Wengine
walitembea kwa siku nyingi kuonyesha ghadhabu yao
kwa kujiondoa katika chama tawala cha CCM kama
wanachama.
"ikiwa
sina ardhi, sina mahala pa kujifungulia watoto wangu,'' alisema Bi Morkelekei
Gume,akitupa kadi yake ya uwanachama wa CCM chini .
"mwanangu
yuko katika shule ya upili, kwa sababu ya nyasi zinazotoka hapa.''
''Ikiwa
wanataka ardhi yangu wanaweza kuniua.''
Mwanamke mmasaai
anashikia bango linalosema "tutapigania ardhi yetu hadi mwisho wake.''
Wanawake hapa ndio wamekuwa wakisikika zaidi katika maandamano yao .
Wanawake
wamekuwa wakisikika zaidi, wameathirika zaidi kutokana na hatua ya serikali
kuwafukuza, wakiachwa bila kazi kuwalea watoto wao kwa hali ngumu wakati
wanaume wakienda katika sehemu za miji ambako wanapata kazi kama
walinzi.
Pia
wameongoza maandamano tangu viongozi wao wa kisiasa waliopinga mpango wa ujenzi
wa barabara waliokuwa wamesema wataondoka katika chama tawala kukosa kutimiza
ahadi zao.
Eneo
la Loliondo lina wanyama wengi wa porini na hivyo kuvutia watalii ingawa sio
wengi. Linapakana na mbuga ya wanyama ya Maasai Mara iliyoko Kenya pamoja na
hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro.
Waziri
wa utalii Khamis Kagasheki anatetea hatua ya serikali kutaka kuwaondoa wamasaai
katika eneo hilo
akisema kuwa mradi huo utasaidia katika kuendeleza uhifadhi kwani Maasai
wametumia ardhi hiyo vibaya.
Lakini wasomi wanasema kuwa jamii ya wamaasai kawaida hawaathiri
wanyamapori.
"nina
swali moja kubwa kwa wanaosema kuwa wamaasai ni tisho kubwa kwa wanyamapori
kuliko kampuni hiyo ya kiarabu ya OBC," alisema Benjamin Gardner wa chuo
kikuu cha Washington
na ambaye amesomea maswala ya ardhi miongoni mwa wamaasai kwa miongo miwili.
Ni nadra kwa wamaasai kuwinda wanyama na
hutumia ardhi kuzuia baadhi ya wanyama kujifungulia huko kwani ni tisho kwa
mifugo wao.
Mashirika
13 ya kijamii kutoka kote nchini Tanzania ,
yamesema kuwa wamaasai, wana vibali vichache sana vya kumiliki ardhi, na kuwa serikali
inawapotosha watu
Viongozi
wa jamii hiyo wanapanga kwenda mahakamani kuishtaki serikali, lakini wanahofia
kuwa huenda swala hilo
likakosa kutatuliwa haraka kwani kuna kesi moja iliyowasilishwa mwaka 2009 na
haijapata ufumbuzi hadi wa leo.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment