Friday, April 26, 2013

Bajeti ya jumuiya ya Afrika Mashariki yatanganzwa, ni Dola za Marekani Mil 177.2
Mahmoud Ahmad, Arusha
Jumla ya kiasi cha dola za marekani million 177,238,966 zimetengwa kwenye bajeti ya jumuiya ya Afrika ya mashariki kwa mwaka wa fedha 2013-14 na kuidhinishwa na baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo kwenye kikao chao cha 26 dharura kilichoisha wiki hii jijini Arusha. 

Mkutano huo ulioanza mnamo tarehe 22-23 kwa ngazi ya wataalamu na kufuatiwa na mkutano wa makatibu wakuu wa nchi wanachama na kupokea hatua zilizofikiwa katika majadiliano ya itifaki ya umoja wa fedha wa jumuiya ya Afrika ya mashariki ambao unatarajiwa kutiwa saini na wakuu wa jumuiya hiyo katika mkutano wao wa 15 mwezi wa november mwaka huu.
 Aidha mkutano huo utajadili pia pendekezo la kuongeza wigo wa mamlaka ya mahakama ya Afrika ya mashariki kwa kupitia mapendekezo yaliojadiliwa kwenye vikao vya wataalamu na makatibu wakuu wa jumuiya hiyo.
 Katika hatua nyingine mkutano huu wa dharura wa 26 wa jumuiya ya Afrika ya mashariki ambao unaisha leo na kuwakutanisha wataalamu na makatibu wakuu kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrka ya mashariki umejadili mambo matatu makuu yatakayopelekwa kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kutia saini.
 Kwa upande mwingine mkutano huu umejadili pia hatua iliyofikiwa katika uandaaji wa itfaki ya hadhi na kinga kwa watumishi wa jumuiya na taasisi zake zote.
MJENGWA BLOG.

No comments:

Post a Comment