Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole-Medeye wakati akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Kilindi Dastan Kitandula (CCM).
Ole Medeye alisema kuwa uamuzi wa kufuta hati miliki hizo kwa
sasa uko mikononi mwa Rais baada ya kukamilika kwa hatua zote.
Katika swali hilo
Kitandula alitaka kujua ni lini Serikai itafuta hati miliki kwa mashamba ya
mkonge ambayo kwa muda mrefu yametelekezwa ili kuwagawia wananchi wenye
uhitaji.
Awali, Herbert Mtangi (Muheza-CCM) alitaka kujua ni viwango gani
stahiki ambavyo wawekezaji wa zao la katani wanatakiwa kulipa kama
ushuru kwa halmashauri husika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa Hawa Ghasia, alisema kuwa halmashauri zote nchini zimepewa mamlaka ya
kutoza ushuru wa mazao chini ya kifungu 7 (1) (g) cha sheria ya fedha za
serikali za Mitaa.
“Ushuru huu hulipwa na mununuzi na unatozwa mahali ambapo zao
linazalishwa na kwa bei ya mkulima yaani bei ya zao kabla ya kuongezwa
thamani,” alisema Ghasia.
Alisema wafanyabiashara wote wa zao la mkonge,wanatakiwa kulipa
ushuru wa mazao ambao ni kuanzia asilimia 3 hadi 5 kwa mujibu wa sheria.
Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge
amemtetea bosi wake, Profesa Jumanne Maghembe kuhusu tuhuma zilizoelekezwa
kwake za kupeleka mradi mkubwa wa maji jimboni kwake, huku wilaya zingine
zikiachwa ‘yatima’.
Akijibu hoja mbalimbali za wabunge jana, Dk Mahenge alisema
mradi wa Mwanga-
Same-Korogwe ni mwendelezo wa miradi mikubwa ya maji kama ule wa Chalinze.
“Yote yaliyoelezwa tutayazingatia. Ni kweli kutokana na unyeti
wa suala la maji, lazima hisia zitapelekea mawazo mengi juu ya kasungura kadogo
kuonekana mtu mmoja amejimegea wengine hakuna,” alisema Dk Mahenge.
Alisema hoja ya fedha hizo kutengwa mara moja, inatokana na
mradi kutakiwa kutekelezwa kwa miezi 18 ili uweze kukamilika kwa muda
uliopangwa.
“Ule mradi tunaugawa sehemu tatu, lengo ni kutakiwa kukamilika
ndani ya muda wa miezi 18 iliyopangwa,” alisema.
Naye Profesa Maghembe alisema hisia za wabunge zilionyesha kuwa
Sh398 bilioni alizoomba hazitoshi kutekeleza miradi ya maji vijijini, hadi
kushawishi bunge kujadiliana na Serikali kupata fedha zaidi.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment