Wasomi nchini Australia
wametaka mpasuaji wa kichina anayetuhumiwa kufanya biashara haramu ya viungo
vya mwili kuvuliwa taji la mtaalamu alilopewa katika chuo kikuu cha cha Sydney .
Huang
Jiefu, aliyesomea taaluma hiyo huko Sydney , hivi
maajuzi aliongezewa muda taji hilo
la kuwa Profesa kwa miaka mitatu inayokuja.
Lakini
wasomi kutoka kitengo cha afya cha chuo kikuu hicho wamemtaja kuwa bingwakwa
jitihada zake katika kuleta mageuzi kwenye taaluam hiyo.
Chuo
kikuu cha Sydney ni mojawapo ya vyuo vikuu
vilivyo na sifa kuu nchini Australia.Mnamo mwaka 2005 Huang Jiefu,alikuwa afisa
mkuu wa kwanza wa afya aliyefichua mtindo wa China kutoa viuongo vya mwili
kutoka kwa wafungwa.
Na
anatazamwa na wengi kama aliyeleta mageuzi
katika katika mfumo huo unaoshutumiwa kwa ukubwa.
Kwa
waliopanga ombi la kutaka apokonywe taji alilopewa wanaona kwamba anahusika na
mfumo huo usio na maadili na amehusika katika hilo kwa kufanya upasuaji wa kutoa ma
kubadili viungo hivyo.
Wanadai
kuwa yeye na maafisa wa serikali Beijing
wametoa malipo ili kusitisha biashara hiyo haramu.
Kw
amujibu wa mashirika ya kutetea haki za binaadamu China huua wafungwa takriban 4000
kila mwaka kwa kutumia sindano yenye sumu ili kutoa viungo hivyo katika miili
ya wafungwa hao.
BBC SWAAHILI
No comments:
Post a Comment