Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Yusuf Kunasa kucheza
nchini Msumbiji.
Shirikisho la Mpira wa Miguu cha Msumbiji (FMF)
lilituma maombi TFF kumuombea hati hiyo Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya
Estrela Vermelha da Beira inayocheza Ligi Kuu nchini humo.
Kunasa ambaye msimu huu hakuwa na timu (free
agent) amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji wa ridhaa (amateur). Zaidi ya
wachezaji kumi kutoka Tanzania
hivi sasa wanacheza katika klabu mbalimbali nchini Msumbiji.
TFF
No comments:
Post a Comment