Uingereza imetangaza kuwa itakoma kutoa msaada kwa Afrika
Kusini kuanzia mwaka 2015.
Waziri katika wizara ya maendeleo ya kimataifa ya Uingereza
Justine Greening
Waziri
wa maendeleo ya kimataifa, Justine Greening, anatarajiwa kutangaza rasmi hatua
hiyo itakayoinyima afrika kusini msaada wa moja kwa moja wa dola milioni
thelathini kila mwaka baadaye hivi leo.
Maafisa
wanasema hatua hiyo ni ya kutambua ustawi wa Afrika kusini tangu kukamilika kwa
utawala wa kibaguzi, huku taifa hilo
likionekana kuwa na uwezo wa kutoa msaada kwa mataifa mengine.
Katika
hatua kama hiyo Uingereza ilisitisha kutoa msaada kwa taifa la India
mwaka uliopita.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment