Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya ambapo ametangaza
majina ya mawaziri wanne. Wanne hao ni pamoja na Dkt. Fred Okeng'o Matiangi
ambaye ni waziri mteule wa Teknolojia na Mawasiliano, Henery Rotich ameteuliwa
wizara ya Fedha, James Wanaina Macharia ndiye Waziri mteule wa Afya na Balozi
Amina Mohammed ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.
Ilitarajiwa
kwamba Rais Kenyatta angewataja mawaziri wote 18, lakini amesema wengine
watatangazwa baadaye na kuomba taifa kuwa na subira. Huku haya yakiarifiwa
Bunge la Kenya
limeidhinisha kamati maalum ambayo itawachuja mawaziri watakaoteuliwa na Rais.
kamati hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.
Chini
ya katiba ya Kenya
sharti bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo Mawaziri,
mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba.
No comments:
Post a Comment