Suala la Afrika kujitawala na
kujitegemea katika nyanja zote limekuwa mjadala wa muda mrefu kutoka kwa
Waafrika wenyewe.
Kwa muda mrefu Bara la Afrika limeonekana kuwa nyuma katika
maendeleo ya uchumi, jamii na siasa.
Baadhi ya wapelelezi wa wakoloni katika
karne ya 18 walilitaja bara hilo kama la giza kutokana na hali ya
kudorora kimaendeleo kulinganisha Ulaya walikotoka.
Licha ya kuja kutawala kwa takriban karne moja, wakoloni kutoka Ulaya wameendelea kuzitawala nchi za Afrika kwa ukoloni mambo leo.
Suala la Afrika kujitawala na kujitegemea katika nyanja zote limekuwa mjadala wa muda mrefu kutoka kwa Waafrika wenyewe.
Licha ya kuja kutawala kwa takriban karne moja, wakoloni kutoka Ulaya wameendelea kuzitawala nchi za Afrika kwa ukoloni mambo leo.
Suala la Afrika kujitawala na kujitegemea katika nyanja zote limekuwa mjadala wa muda mrefu kutoka kwa Waafrika wenyewe.
Mjadala huo umeibuka pia katika tamasha la tano la Kigoda cha
Mwalimu Nyerere, ililofanyika hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam likiwa
limebeba ujumbe wa “Maendeleo ni mapambano ya Ukombozi,” suala la Afrika
kujitawala limetawala.
Akitathmini falsafa ya maendeleo ya Mwalimu Julius Nyerere,
Profesa Manuh Takyiwaa kutoka chuo Kikuu cha Ghana , Legon anasema pamoja na
Afrika kuwa na maliasili nyingi, bado wapo viongozi ambao wanazigombania kwa
lengo la kujinufaisha wao binafsi huku wakiwaacha wananchi mikono mitupu.
Anahoji falsala ya kujitegemea na kama
rasilimali yaani watu, ardhi, siasa safi
na uongozi bora zinatumika ipasavyo.
“Waafrika bado wanagombania maliasili zao, nyingine zikichukuliwa na kusafirishwa nje kwenda kuyanufaisha mataifa ya mbali. Hata kitendo cha kuikumbatiaChina
kinaonyesha kuwa hatuja jifunza chochote,” anasema Takyiwaa.
“Waafrika bado wanagombania maliasili zao, nyingine zikichukuliwa na kusafirishwa nje kwenda kuyanufaisha mataifa ya mbali. Hata kitendo cha kuikumbatia
Naye Profesa Penina Mlama kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam ,
anatoa mfano wa utegemezi wa Watanzania kiasi cha kuwataka hata wahisani
wachangie ujenzi wa vyoo vya shule.
“Shule nyingi vijijini hazina vyoo… Nimekutana wa wakuu wa shule wanaosema tunasubiri wahisani watusaidie. Nini kinachotufanya tuwasifu na kuwatetemekea baadhi ya viongozi ambao tunajua kabisa wanalimaliza taifa letu?”
“Shule nyingi vijijini hazina vyoo… Nimekutana wa wakuu wa shule wanaosema tunasubiri wahisani watusaidie. Nini kinachotufanya tuwasifu na kuwatetemekea baadhi ya viongozi ambao tunajua kabisa wanalimaliza taifa letu?”
Profesa Mlama kwa upande mwingine anasema hali imekuwa mbaya
zaidi hata kwa baadhi ya wasomi, ambao wamekuwa wakifundisha njia sahihi ya
kufuatwa huku wakiwanyooshea vidole wengine, lakini hivi sasa wameanza kwenda
kando na kuanza kuyatenda yale waliyokuwa wakiyapinga.
“Tunapozungumzia mustakabali ukombozi wa kimaendekeo ni lazima
tupate suluhisho la hii nguvu inayoleta haya yote. Watu wapo, lakini ni wa aina
gani?”
Kwa upande wake Profesa Monica Lima e Souza kutoka Chuo Kikuu
cha Federal cha Rio Dejaneiro, anatoa uzoefu wa Brazil ambayo imepiga hatua katika
kujikomboa kwa kuanzisha mtalaa wa masomo katika vyuo vikuu unaolenga
kujikomboa kimaendeleo kupitia fikra za Kiafrika.
“Tusiwe na mwelekeo mmoja katika kufikia malengo yetu.
Tunazungumzia bara nzima, turuhusu mawazo tofauti kutoka kila kona ili tuwe na
nguvu ya kufika kule twendako,” anasema Souza.
“Wanasema
Naye Profesa Thandika Mkandawire kutoka Shule ya Uchumi ya
Uingereza, aliyekuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo anasema baadhi ya viongozi wanadhoofisha
kwa makusudi jitihada za kuiletea maendeleo Afrika.
Anaongeza kuwa japo wazo la kuiunganisha
Afrika lilikuwa na nia ya kulipa nguvu ya kiuchumi bara hilo , lakini kinachofanyika hivi sasa ni
kinyume na dhana nzima ya waasisi wake.
“Katika mashirikisho mbalimbali ya nchi hivi sasa, ajenda zao ni tofauti kabisa na zile za kulikomboa bara la Afrika,” anasema Mkandawire.
“Katika mashirikisho mbalimbali ya nchi hivi sasa, ajenda zao ni tofauti kabisa na zile za kulikomboa bara la Afrika,” anasema Mkandawire.
Anaongeza kuwa Bara la Afrika linauwezo,
nguvu na maarifa ya kujitawala lenyewe na siyo watu kutoka nje kuja kuchuma
maliasili na kuondoka na utajiri mkubwa huku watu wake wakigeuka vibaraka
wanaowanaoshuhudia tu kinachoendelea.
“Hatuhitaji watu wapya kutoka nje, bali tunahitaji watu wapya kutoka hapa hapa,” anasema Mkandawire.
“Hatuhitaji watu wapya kutoka nje, bali tunahitaji watu wapya kutoka hapa hapa,” anasema Mkandawire.
Licha ya kuhimiza mapambano ya Afrika
kwa vijana, Mkandawire ameonyesha wasiwasi kwa vijana wa sasa.
“Ni kweli kuwa vijana wanahitajikasana ,
lakini je, wapo hao wenye uwezo?” anahoji Mkandawire.
“Ni kweli kuwa vijana wanahitajika
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa UDSM,
Profesa Rwekaza Mukandara anamtaja Rais wa Misri, Mohamed Morsi kuwa ni
mfano wa viongozi wa Afrika wasio na maono na bara hilo.
Anasema wakati Morsi anaapishwa alitoa hotuba yake ya dakika 15, lakini hakutaja jambo lolote kuhusu bara la Afrika.
Anasema wakati Morsi anaapishwa alitoa hotuba yake ya dakika 15, lakini hakutaja jambo lolote kuhusu bara la Afrika.
Kwa upande wake Profesa Mshumbusi
Kiboyonga wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam anasisitiza kuwa Afrika siyo bara maskini bali
wakoloni ndiyo cha umaskini huo.
“Afrika siyo maskini. Matatizo yetu yamefanywa mtaji na mataifa mengine.Kama wana nia ya dhati, kwanini wameleta mpango wa
kupunguza umaskini na si kuondoa umasiki” anahoji.
“Afrika siyo maskini. Matatizo yetu yamefanywa mtaji na mataifa mengine.
Akizungumzia elimu inayotolewa Afrika na
mfumo mzima wa mitaala anasema nacho ni chanzo kingine cha Waafrika kushindwa
kujikomboa kiuchumi kwani imejaa kifra za kigeni.
“Hatuna chuo chochote Afrika kinachofundisha Uafrika, kufikiri na kuendelea Kiafrika.
Tanzania
ni nchi tajiri kuliko nchi yoyote Ulaya. Utajiri wa Afrika ni watu na mali
zao.Tukiwaweka pamoja, bara hili tutafika tunakotaka kwenda,” anasema
Kiboyonga.
“Hatuna chuo chochote Afrika kinachofundisha Uafrika, kufikiri na kuendelea Kiafrika.
Naye Diana Kamara wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere licha ya
kutambua kuwa ukombozi wa maendeleo ni mapambano yanayoanza ndani ya mtu,
baadhi ya viongozi wa Afrika walijaribu kuvaa ngozi ya kondoo ili kutaka
kuihadaa jamii wanayoitawala kuwa wao ni Waafrika asili kwa mavazi wanayovaa.
“Wapo wanaovaa vitenge au kofia kama
Mobutu aliyekuwa anavaa kofia ya ngozi ya chui, lakini hakuwa na nia ya dhati
ya kulikomboa bara hili. Lazima tuwe Waafrika kutoka moyoni,” anasema Kamara.
Naye Profesa Mathew Luhanga akichangia mjadala huo anasema ili
kuhakikisha kuwa taifa linatimiza malengo yake ya kujikomboa ni lazima kuwe na
uhusiano mzuri kati ya watunga sheria na wasomi.
“Kuna pengo kubwa kati ya watunga sheria na wasomi, hiki nacho
ni kikwazo kwa maendeleo,” anasema Profesa Luhanga.
No comments:
Post a Comment