Saturday, April 20, 2013

Msichana mwingine abakwa nchini India.


Polisi nchini India wamemkamata mwanamme mmoja kwa kuhusika na kumbaka msichana wa miaka mitano katika mji mkuu, Delhi.

Msichana huyo aliumia vibaya na sasa anatibiwa hospitali akiwa mahtuti.
Mshukiwa, mwenye umri wa zaidi ya miaka 20, alikamatwa katika jimbo la Bihar zaidi ya kilomita 1000 kutoka Delhi.
Anatuhumiwa kuwa alimnyakua mtoto huyo karibu na kwao na alimzuwia kwa siku mbili.
Jumamosi maandamano kadha yalifanywa mjini Delhi.
Baadhi ya waandamanaji walieleza hasira kuhusu uhalifu huo.
Wengine waliwalaumu polisi kwa jinsi walivoshughulikia kesi hiyo.
Hilo ni tukio la karibuni kabisa katika visa kadha vya ubakaji ambavyo vimezusha hamasa nchini India.
BBC Swahili

No comments:

Post a Comment