Friday, April 26, 2013

Ligi ya soka daraja la pili Dar es Salaam kumalizika kesho


LIGI Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora, inamalizika kesho ambapo timu tatu zitakata tiketi ya kucheza hatua ya Kanda ili kupata nafasi ya kusaka nafasi ya kucheza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Mohamed Mharizo, amezitaja mechi zitakazochezwa leo kuwa ni Red Coast itakayomenyana na Day Break kwenye uwanja wa Kinesi, wakati kwenye Uwanja wa Makurumla, Friends Rangers wao watakuwa wakichuana vikali na Sharif Stars, huku kwenye Uwanja wa Airwing, Boom FC itakuwa ikikabiliana na Abajalo.
Hadi sasa Red Coast inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 8, ikifuatiwa na Abajalo yenye pointi 7, wakati Sharif Stars inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 6.
Friends Rangers wao wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 5 huku Day Break wakiwa na pointi 3 na Boom FC ikishika mkia kwa kujikusanyia pointi 2.

No comments:

Post a Comment