Arusha: Kushikiliwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema),
Godbless Lema kumeendelea kuibua sokomoko baina ya polisi kwa upande mmoja na
wafuasi wa Chadema na familia yake kwa upande mwingine.
Arusha. Lema aliyekamatwa usiku wa manane kuamkia Ijumaa wiki hii,
alihojiwa kwa saa tatu mfululizo katika Kituo Kikuu cha Polisi, Arusha lakini
alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba kuachiwa kwake kungehatarisha amani.
Akizungumza na gazeti hili kabla ya kujisalimisha kwa askari hao
usiku huo wa kuamkia juzi, Lema alithibitisha kuwapo kwa polisi nje ya nyumba
yake:
“Wapo nje ya nyumba yangu, wanatishia kupiga mabomu kama nisipotoka nje, lakini wanajadiliana na walinzi
wangu na mimi nimewataka wanipe hati ya kunikamata,”alisema.
Wakili wa Lema, Humphrey Mtui alisema mahojiano ya mteja wake na
polisi yalidumu kwa zaidi ya saa tatu kuanzia saa 7:50 mchana hadi saa 11:15
jioni, na kwamba walitaka ufafanuzi kwenye hoja tatu walizodai kwamba
zilijengwa kwenye kauli alizotoa Lema wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi
wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA).
Maneno hayo yanayotafsiriwa na polisi kuwa ni uchochezi ni
pamoja na “Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni woga” na “Nimepata
taarifa kuwa ndani ya dakika 15 Mkuu wa Mkoa atafika, asipofika ndani ya muda
huo nitawaongoza kwenda kudai haki yenu ya msingi ya kupatiwa ulinzi.”
Kauli nyingine ni “Hawa ndio viongozi wetu (akimaanisha mkuu wa
mkoa), tunaowategemea wanakuja kwenye matatizo wakijivuta utafikiri wanakwenda
kwenye send-off.”
Lema anadaiwa kutamka maneno hayo baada ya Mulongo kugoma
kuzungumza na wanafunzi kisha kurejea ndani ya gari akitaka viwepo vipaza
sauti, kitendo kilichowafanya wanafunzi kuanza kumzomea kabla polisi kuanza
kulipua mabomu ya machozi na kumwondoa eneo la tukio mkuu huyo wa mkoa.
Lema na Mulongo wote walikwenda IAA kutokana na tukio la kuuawa
kwa kuchomwa kisu kwa aliyekuwa mwanafunzi wa taasisi hiyo, Henry Kago.
Baada ya vurugu hizo Mulungo alimtuhumu Lema kuandaa mazingira
ya yeye kuzomewa .
Wakati hayo yakiendelea, askari katika kituo anakoshikiliwa Lema
jana asubuhi walivutana vikali na ndugu wa mbunge huyo pamoja na uongozi wa
Chadema Mkoa wa Arusha baada ya kumpa dakika moja kunywa chai aliyoletewa na
kukataa asipewe dawa ya meno kutoka kwa mkewe, Neema.
Habari ambazo gazeti hili lilizipata zinasema kutokana na hali
hiyo, uongozi wa Chadema ulilazimika kumtuma wakili wa Lema, Method Kimomogoro
kwenda Kituo cha Kati cha Polisi Arusha kujua sababu za polisi kufanya hivyo.
Mmoja wa ndugu wa Lema alisema polisi walimpa mbunge huyo dakika
moja tu kunywa chai na kwamba muda huo ulipokwisha walimwongezea dakika
nyingine tatu na kwamba zilipomalizika walimwamuru arejee mahabusu.
Wakati polisi wakifanya hivyo, tayari walikuwa wamekataa asipewe
dawa ya meno aliyopelekewa na mkewe, Neema na kwamba matukio hayo yalizua
mvutano mkali baina yake (Lema) na polisi waliokuwa kituoni hapo.
Mdee, Nassari kukutana na Mulongo
Katika hatua nyingine, wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) kesho wamepanga kwenda kuonana na Mulongo kuzungumza naye kuhusiana na kilichotokea IAA na kusababisha kukamatwa kwa Lema.
Katika hatua nyingine, wabunge wawili wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) kesho wamepanga kwenda kuonana na Mulongo kuzungumza naye kuhusiana na kilichotokea IAA na kusababisha kukamatwa kwa Lema.
Nassari aliliambia gazeti hili jana kwamba wameamua kutoka Dodoma hadi Arusha kwa ajili ya “kushughulikia suala hilo .”
“Jumatatu tunatarajia kuonana na mkuu wa mkoa na tayari nimempa
taarifa. Tunataka kuzungumza naye kilichotokea na hali ya kisiasa kwa sasa
Arusha,”alisema Nassari.
Alisema wao kama wabunge,
hawawezi kukaa kimya wakati kunaonekana kuna mgogoro baina ya mkuu huyo wa mkoa
na mbunge mwenzao, Godbless Lema ambao unakiuka haki za kibinadamu.
“Tutazungumza naye na tutatoa ushauri
wetu …na mimi kama mbunge wa Mkoa wa Arusha, nadhani nina nafasi ya kushauriana
na mkuu wa mkoa kuhusiana na hali ya mambo ilivyo sasa Arusha,”alisema Nassari
na kuongeza:
“Kabla ya kuonana na mkuu wa mkoa, tutajitahidi kuonana na polisi pia kuhusiana na kesi ya Lema na tunataka sisi kama wabunge tuwe sehemu ya wadhamini wa Lema.”
“Kabla ya kuonana na mkuu wa mkoa, tutajitahidi kuonana na polisi pia kuhusiana na kesi ya Lema na tunataka sisi kama wabunge tuwe sehemu ya wadhamini wa Lema.”
Hata hivyo, juhudi za kumpata jana mkuu wa Mkoa wa Arusha,
kuelezea kama amepokea ujumbe kutoka kwa
wabunge hao, zilishindikana kutokana na kuwa katika mapokezi ya marais watano
wa nchi za Afrika ya Mashariki.
Chadema kumzomea RC
Katika hatua nyingine, Chadema mkoani Arusha kimeahidi kwamba kitaendeleza zomeazomea kwa mkuu wa mkoa huo, Mulongo kila watakapomwona kwenye matukio na shughuli zote za kijamii.
Katika hatua nyingine, Chadema mkoani Arusha kimeahidi kwamba kitaendeleza zomeazomea kwa mkuu wa mkoa huo, Mulongo kila watakapomwona kwenye matukio na shughuli zote za kijamii.
Katibu wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema
wafuasi wa chama hicho wataendelea kumzomea Mulongo kila watakapomwona hadi
pale atakapobadilika kifikra, kimwenendo, maneno na vitendo kuhusiana na
uhalali wa Chadema na viongozi wake katika uongozi wa umma waliokabidhiwa
kisheria.
“Kama kupigiwa makofi na
kushangiliwa anapofanya vyema kazi yake,
vivyohivyo mkuu wa mkoa ategemee kukumbana na zomeazomea kubwa
kuliko aliyopata Uhasibu iwapo hatabadilika kiutendaji kwa kufanya kazi za
kisiasa badala ya kuhudumia umma wote bila kujali tofauti za kiitikadi
kisiasa,” alisema Golugwa.
Katika mkakati wake, Chadema kimetishia kumburuta mahakamani
Mulongo kwa tuhuma za kuzusha uongo na kumtishia Lema kwa maneno makali.
“Mawakili wetu wanaendelea na utaratibu wa kufungua kesi ya
kumshtaki mkuu wa mkoa kwa kosa la kumtishia kwa maneno makali Lema na pia
kutoa maneno ya uzushi, upotoshaji na uongo,”alisema Golugwa.
Chadema pia walisema askari polisi waliomkamata Lema hawakuwa na
kibali cha ofisi ya Spika wala hati ya kukamata kutoka kwa ofisa wa jeshi hilo kama sheria
inavyoelekeza.
CCM Arusha
Wakati huo huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Isack Joseph jana alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka juu ya kifo cha mwanafunzi wa IAA ili haki iweze kutendeka.
Wakati huo huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Isack Joseph jana alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka juu ya kifo cha mwanafunzi wa IAA ili haki iweze kutendeka.
MWANANCHI
hi
No comments:
Post a Comment