Chama cha soka nchini Uingereza, FA kimenuia
kumpa adhabu kali mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez kwa kitendo chake cha
kumng'ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika mchezo wa jumapili baina ya
Liverpool na Chelsea,mchezo uliomalizika kwa
sare ya 2-2.
FA
imesema mwamuzi wa mchezo huo hakukiona kitendo hicho uwanjani lakini marejeo
ya picha za mchezo huo zilionyesha Suarez alimng'ata Ivanovic,kitendo ambacho
kinachukuliwa kama vurugu mchezoni na adhabu
yake ni kufungiwa mechi tatu lakini adhabu hiyo haitoshi kwa tukio alilolifanya
Suarez.
Suarez
amepewa muda wa mpaka saa 12 jioni jumanne ya April 23, awe amekubali au
kukataa kosa hilo kabla ya tume ya kudhibiti
maadili haijakutana hapo siku ya jumatano kutoa hukumu stahili kwa kosa hilo .
Mwenyewe
Suarez aliisha kiri kufanya kosa hilo na
kumuomba Ivanovic msamaha kwa njia ya simu na kuwaomba mashabiki wa soka
wamsamehe kwa kosa hilo .
Klabu
yake ya Liverpool imempa adhabu ya kumpiga faini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay .
Mwaka
2010, Suarez wakati akiichezea Ajax ya Uholanzi
alimng'ata begani kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal na kufungiwa mechi saba
na chama cha soka nchini Uholanzi kwa kosa hilo .
Itakumbukwa
Suarez tayari amekwishawahi kufungiwa kutocheza mechi nane za mashindano nchini
Uingereza na faini ya paundi elfu 40 kwa kosa la kumtolea lugha ya kibaguzi
beki wa Manchester United Patrice Evra mwaka 2011.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment