Umoja wa Mataifa umemteua Generali mmoja raia wa Brazil ambaye anasifika kwa kudhibiti mtaa mmoja
wa mabanda nchini Haiti
kutokanamana na vurugu kuweza kuwaongoza walinda amani wa Umoja wa Mataifa
katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo .
Generali Carlos Alberto dos Santos Cruz ataongoza kikosi cha
wanajeshi 20,000, ikiwemo kikosi kipya cha wanajeshi kitakachopambana na waasi
mashariki mwa nchi.
Hii ndio mara ya kwanza kwa Umoja wa mataifa
kukabidhi kikosi cha wanajeshi nguvu kuweza kupambana na waasi.
Generali
Santos Cruz, aliambia BBC kuwa wanajeshi wake, watafunzwa namna watakavyo
pambana na waasi bila kuwajeruhi raia na kuharibu mali
nchini Congo .
"eneo
tete zaidi siku hizi ni Mashariki mwa nchi,'' Cruz alimbia BBC
"niko
tayari kukabiliana, na hali ngumu zaidi. Lengo kuu ni kuwaondolea hali ngumu
wanayokabiliana nayo watu wa Congo .''
Generali
Santos Cruz ataongoza kikosi cha wanajeshi 2,500, wakiwa na jukumu la
kuwapokonya silaha waasi pamoja na kuwarejesha katika maisha ya kiraia
Mashariki mwa DR Congo.''
Kikosi
cha walinda amani cha Umoja wa mataifa,kilichoko Congo
kimekosolewa sana
kwa kukosa kumaliza vita, vya miongo miwili.
Wanajeshi
kutoka Tanzania , Malawi , Msumbiji na Afrika Kusini ndio walio
wengi katika kikosi hicho na wataanza kazi yao mwezi Julai.
Generali
Santos Cruz ni kamanda mstaafu, wa kikosi kilichowahi kutumwa nchini Haiti , na
anasifiwa kwa kupambana vikali na megenge ya majambazi nchini Humo mwaka 2007
BBC
SWAHILI
No comments:
Post a Comment