Sunday, April 21, 2013

Dola Mlioni 16 kusaidia mradi wa maji Mkoani Manyara.


Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa (kulia) akibadilishana mkataba na Mkurugenzi  wa OFID kushoto ni Katibu wa Waziri wa Fedha, Omar Khama akiwasikiliza wafanyakazi wa OFID.


Serikali ya Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya dola za kimarekani milioni 16 kusaidia mradi wa maji Orkesumet mkoani Manyara. Mkataba huo umesainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na OPECFund For International Development (OFID) wakishirikiana na BADEA. OPEC wametoa milioni 8 na BADEA wametoa milioni 8. Ili kufanikisha mradi  huu Serikali ya Tanzania itatoa dola za kimarekali milioni 2.42, Hivyo kufanya mradi huu kufikia jumla ya dola za Kimarekani milioni 18.42.

Chanzo: Ingiahedi Mduma, DC Washington


No comments:

Post a Comment