Asalam Allaykum ndugu zangu,
Siku ya jumapili kama mnaishi katika familia ya watu kidogo ni vema muende kufuturu hotelini. Lakini kama mna uwezo, ila kwa wale wenzangu na mimi ambao ATM hazisomi tutakula Mihogo, Vibibi, Chapati, Maharage ya nazi, Samaki wa kukaanga, vitumbua na kachori.
Chai ya mkandaa (black tea), matunda aina kama tatu ama mbili na maji meeengi. Haina haja kutengeneza juice kwa maana matunda na maji yanatosha kuwa juice.
NB: Kwa wale wasiofahamu vibibi, ni mfano wa (pancake) ambapo unasaga mchele, unachanganya na tui la nazi, kisha unaweka katika kigae (mfano wa frying pan iliyotengenezwa kwa udongo kama kijungu) halafu baada ya kukauka na kuwa pancake, unaiweka katika tui la nazi ambalo lina sukari na hiliki. unaweka jikoni kwa muda kidogo ili iive pamoja na nazi hiyo, ukishaiweka katika sahani ikapoa inakuwa vibibi)
No comments:
Post a Comment