Sunday, August 5, 2012

Futari ya leo,

Asalam Allaykum wadau,

Leo tutakula futari adhiiwm kutoka Zanzibar kwenye kabila la kingazija, tutakula mkate wa ufuta, mkate wa sinia (kumimina), mbaazi za nazi, nyama za kukausha na viungo, maandazi (mahamri), ndizi mbivu za nazi (mkono wa tembo), muogo wa nazi na samaki.

Apple (tufaha), nanasi na tikiti maji (water melon) yatakuwa matunda yetu ya leo. Zingatia: Utaona narudiarudia sana tunda la tikiti maji, sababu ni kuwa mwili wa binaadamu unahitaji sana maji,na tukifunga siku nzima tunashinda na kiua, kwa hivo tunda hili husaidia sana kumpa mwanadamu maji mengi.

Shukran,

No comments:

Post a Comment