OFISI YA TAIFA YA
TAKWIMU YATOA TAARIFA YA HALI YA UCHUMI , PATO LA TAIFA LA TANZANIA LAKUA.
Na. Aron
Msigwa – MAELEZO.
3/8/2012. Dar
es salaam .
Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa taarifa ya hali ya uchumi nchini na kufafanua
kuwa pato la taifa la Tanzania limekua kwa asilimia 7.1 katika kipindi cha
robo ya mwaka 2012 ikilinganishwa na asilimia 6.1 za mwaka jana.
Ukuaji huo
wa asilimia 7.1 unatokana na ongezeko la uzalishaji katika shughuli mbalimbali
za kiuchumi zikiwemo za kilimo, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi na zile za utoaji wa
huduma mbalimbali za jamii.
Akitoa
taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa lengo la utoaji wa taarifa hizo kwa
vipindi vifupi vya vya robo
mwaka unalenga kuwapatia wadau wa Takwimu za Pato la Taifa uwezo wa kutathmini
mabadiliko ya ukuaji wa uchumi nchini.
Amesema
kuwa jumla ya thamani ya pato la Taifa katika kipindi cha robo ya mwaka 2012 ni
shilingi 4,220,535 milioni ikilinganishwa na kiasi cha shilingi milioni
3,940,261 za mwaka 2011.
Amefafanua
kuwa ukuaji wa shughuli uzalishaji katika shughuli za kilimo nchini ulifikia
asilimia 1.4 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2012 zikilinganishwa na
asilimia 1.2 katika kipindi hicho kwa mwaka 2011 kutokana na upatikanaji wa
mvua za kutosha nchini katika mikoa inayozalisha mazao kwa wingi.
Amesema
ukuaji katika shughuli za uvuvi ulikua asilimia
2.6 katika robo ya kwanza ya mwaka 2012 huku shughuli za uchumi katika sekta ya
viwanda na Ujenzi ambayo inahusisha uchimbaji wa madini na kokoto ikikua kwa
asilimia 14.3 ikilinganishwa na 0.8% za mwaka 2011.
Bw. Oyuke
ameongeza kuwa ongezeko hilo la uzalishaji wa madini ya
dhahabu linatokana na uzalishaji wa wa madini ya dhahabu kutoka kilo 8,140 kwa
mwaka 2011 hadi kufikia kilo 16,736 kwa mwaka 2012.
Pia
amebainisha kuwa shughuli za utoaji wa huduma za biashara za jumla na
rejareja, ukarabati wa magari na pikipiki na vifaa vingine vya majumbani katika
kipindi hicho zilifikia asilimia 9.0 huku shughuli za upangishaji nyumba na
biashara zikiwa 8.2 %, uchukuzi na mawasiliano 16.4%, hoteli na migahawa 3.8%,
Benki asilimia 15 shughuli za uendeshaji serikali
6.4%, Elimu 6.1% na utoaji wa huduma za Afya nchini zikikua kwa kasi ya
asilimia 5.1.
Hata mimi nimekua...Mhhhhhhhh.....
No comments:
Post a Comment