WANANCHI waishio mpakani
mwa Tanzania na Uganda
wameingia na hofu baada ya kugundulika kuwa ugonjwa hatari wa Ebola imeingia
nchini.
Watu wengi mkoani hapa
kuanzia juzi walionekana kuingiwa na wasiwasi baada ya taarifa kuzagaa kuwa
mgonjwa mmoja amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Karagwe ya Nyakahanga,
mkoani hapa.
Wengi walisikika
wakishauri serikali za Uganda
na Tanzania
kushirikiana kudhibiti ugonjwa huo usizidi kusambaa zaidi.
Inaelezwa kuwa mgonjwa
huyo aliingia nchini akitokea nchi ya Uganda na kwamba hivi sasa amelazwa
katika Hospitali ya hiyo chini ya uangalizi maalumu wa madaktari.
Wananchi wazungumza
Wananchi hao walisema
kuwa katika maeneo kama Mutukula ni vigumu sana kudhibiti mtu mwenye ugonjwa
asiwaambukize wengine kutokana na mwingiliano mkubwa wa kibiashara uliopo.
Mkulima katika eneo hilo
lililopo Wilaya ya Missenyi, Samihu Majidu alisema kuwa tangu walipotangaziwa
kuchukua tahadhari, wanaishi kwa wasiwasi, wanaogopa kugusana na kushikana
mikono.Naye, Sauda Hassan, Mtanzania anayefanya biashara katika eneo la
Mutukula alisema
kuwa hata kama watakuwa makini kivipi, lakini bado vyombo vya
usafiri ni tatizo kubwa linaloweza kueneza ugonjwa huo kwa kasi.
“Wenyewe mnaona hali
ilivyo, watu wa Mbalala, Busia (Uganda )
wako hapa, kama mtu ana ugonjwa utazuiwa
vipi?” alihoji.
Aliongeza: “Wanakuja
wamebanana kwenye magari wakati tunaambiwa msigusane, magari yanajaza sana abiria wengine
wanasimama.”Sauda alisema: “Tunafanya biashara hapa, mteja anakuja anakupa hela
unashika bila kinga yoyote kama mteja ana
ugonjwa ukashika hela ambayo ina majimaji utaugua, Nadhani tununue mipira ya
kuvaa mikononi wakati wa kufanya biashara maana tukisema tuache biashara uchumi
utashuka.”
Alisema hata kama Serikali itafunga mpaka wa nchi hizo bado tatizo litakuwepo
kutokana kuwepo kwa njia nyingi za panya.
Akizungumza na
Mwananchi Jumapili jana, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Nyakahanga, Dk Andrew
Cesari alikiri kupokea mgonjwa mwenye dalili zinazowiana na za ugonjwa wa
ebola.
Alisema mgonjwahuyo alipelekwa hospitalini hapo akitoka eneo la Kyerwa ambalo lipo mpakani na nchi hiyo yaUganda .
Alisema mgonjwahuyo alipelekwa hospitalini hapo akitoka eneo la Kyerwa ambalo lipo mpakani na nchi hiyo ya
Dk Cesari alisema kuwa
mgonjwa huyo alikuwa ana homa kali, alivuja damu sehemu mbalimbali za mwili
wake na kutaapika.
Daktari huyo alisema kwa
mujibu wa maelezo ya ndugu zake, mgonjwa huyo alianza kupatiwa matibabu
nyumbani kwao na alipoonekana kuzidiwa ikibidi wampeleke hospitalini hapo.
Alisema mgonjwa huyo alipokelewa katika chumba maalum na kupelekwa katika wodi ya magonjwa hatari ambapo ametengwa na anaendelea vizuri. “Damu sasa imesimama kutoka, ameacha kutapika, lakini bado hatujajiridhishakama
ugonjwa alio nao ni Ebola maana yapo magonjwa mengine yanayoweza kumfanya awe
na dalili hizo,” alisema.
Alisema mgonjwa huyo alipokelewa katika chumba maalum na kupelekwa katika wodi ya magonjwa hatari ambapo ametengwa na anaendelea vizuri. “Damu sasa imesimama kutoka, ameacha kutapika, lakini bado hatujajiridhisha
Alisema dalili za awali
za mgonjwa wa Ebola ni homa, uchovu wa viungo, mafua, koo kuwasha, kutapika na
kuharisha.
No comments:
Post a Comment