AZAM FC imetoa nafasi ya
pili kwa Yanga, kumrejesha nyota wake wa zamani, Mrisho Ngassa- ambayo ni kutoa
dola za Kimarekani 50,000 (zaidi ya Sh. Milioni 80) ili irejeshewe mchezaji
huyo, ambaye kwa sasa ametolewa kwa mkopo Simba SC . Soma taarifa hii ya Azam,
ambayo BIN ZUBEIRY imetumiwa na Meneja wa klabu hiyo,
Patrick Kahemele,
**
Ufafanizi juu ya suala
la mchezaji Mrisho Halfani NgasaKlabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya
ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekana kupotoshwa
- Azam FC
ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya
Jumatano 1/08/2012 saa saba mchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na
mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopo kwenye
kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo
iliyopangwa ilikuwa ni Dola 50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa
makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwa ilikuwa
tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa
kubwa zaidi ya mwenzake.
Kwa maana hiyo biashara
ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni
kutoa haki kwa kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.
Pia tunaomba ifahamike
bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa
asaidie kushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka
bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyote ambayo Azam FC itaona imekidhi
mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FC
yazingatiwe.
- Hadi
kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba
pekee iliyojibu kwa maandishi na kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga
wao hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbe wao wa
Kamati ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya
zaidi ya milioni 20. Na Yanga haikuwa tayari kuboresha ofa yake.
- Muda wa
kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia
kwa makamu Mwenyekiti wake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo
waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yanga hawakuonekana
na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana
interest.
- Kikao
cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa
ilishindikana kutokana na kutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000.
Kwa maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo kwenye klabu
iliyofika na kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)
- Simba
walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh
2,000,000) pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba
- Sababu
za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam
FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki.
- Azam FC
inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama
inavyopotoshwa. Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado
wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya
kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC
- Tunaomba
kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba
wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda
tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu.
- Lakini
Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya
uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC
haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa
nidhamu.
- Kwa
Sakata hili limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo.
Naomba nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za
kuchagua baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa
safarini Mwanza.
- Kupelekwa
kwa mkopo Moro United?
- Kupatikana
kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40
- Kukubali
adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati
akitumikia adhabu.
Redondo alithibitisha
kuipenda Azam FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia
adhabu yake na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya
wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu sana. Azam FC inajivunia kuwa na
mchezaji kama Redondo na bila kupepesa macho wala kung’ata maneno. Azam FC
inamchukulia Redondo kama mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake
na inamtaka aendelee kuwa na moyo huo.
Imetolewa na utawala.
Azam FC
No comments:
Post a Comment