Polisi wa Ugiriki wamewakamata watu karibu 5,000, kwenye
operesheni dhidi ya wahamiaji haramu, huku kukiwa na wasi-wasi kuwa wakimbizi
kutoka Mashariki ya Kati, wanaweza kutaka kuingia kwa sababu ya vita vya Syria .
Watu zaidi ya 1,000 wamekamatwa hadi sasa, na
wengine zaidi wanatarajiwa kuzuwiliwa.
Wahamiaji
wasiokuwa na nyaraka zinazofaa watarejeshwa makwao.
Zaidi
ya 80% ya wahamiaji wanaoingai Umoja wa Ulaya, wanapitia Ugiriki.
Na
baadhi ya wanasiasa wameitaka serikali ichukue msimamo mkali kuhusu wahamiaji
haramu, wakati Ugiriki inapita kwenye msuko-suko mkubwa kabisa wa kiuchumi kwa
miongo kadha.
Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment