Friday, August 3, 2012

Futari ya leo,

Asalam allaykum,

Leo tutapika futari murua kabisa ambayo itakuacha ukijiramba vidole mpaka ushindwe kunawa mikono yako baada ya kula.

Tutakuwa na ndizi mbivu za nazi (mkono wa tembo), mihogo ya nazi, chapati na mchuzi wa maini. Samaki wa kukaanga, sambusa, ghajia na katles. Matunda leo tutakuwa na machungwa na tikiti maji (water melon).

Chai ya maziwa na juice ya mananasi iliyochanganywa na maembe mabichi.

No comments:

Post a Comment