Wizara ya Maliasili na
Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake tisa (9) kufuatia kadhia
ya utoroshaji wa Wanyamapori Hai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao
wamechukuliwa hatua husika kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma
zilizokuwa zikiwakabili.
(1) Waliofukuzwa kazi
kutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:
- Bw. Obeid F. Mbangwa -
Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi
Matumizi ya Wanyamapori,
- Bw. Simon Charles
Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,
- Bw Frank Mremi - Ofisi
ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.
(2) Aliyeondolewa Cheo
cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza
kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama ni:
- Bw. Bonaventura M.C.
Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuia Ujangili.
(3) Wafuatao ni Maafisa
Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya Wakuu wao wa kazi yaliyo
kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la Maandishi:
- Bibi Martha P. Msemo -
Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.
- Bibi Anthonia Anthony
– Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam .
(4) Bw. Silvanus Atete
Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha
aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu
mtumishi wake aliyekiuka Sheria katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka
kwa Katibu Mkuu taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.
- Silvanus Atete Okudo –
amepewa Onyo Kali la Maandishi.
(5) Wafuatao ni Maafisa
ambao uchunguzi dhidi yao
unaendelea:
- Bw. Mohamed Madehele –
Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori
- Bibi Mariam Nyallu –
Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.
Wahusika wengine katika
kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watachukiliwa
hatua na mamlaka nyingine husika.
Mhe. Khamis Suedi
Kagasheki
WAZIRI WA MALIASILI NA
UTALII
13 Agosti 2012
Imetolewa kwenye Press
Conference iliyofanyika Katika Viwanja vya Bunge Dodoma tarehe 13 Agosti 2012)
No comments:
Post a Comment