Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama
(aliyeshika mwenge) akielezea miradi ya maendeleo
itakayozinduliwa, kufunguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi kupitia
Mwenge wa Uhuru mkoani Kilimanjaro.( Picha na Ofisi ya RAS Kilimanjaro).
Na: Epifania Temu – RS Kilimanjaro
Mkoa wa Kilimanjaro umeonesha nia na juhudi za kupambana
na tatizo la uingizaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa na
kuwakamata wahusika wa uhalifu huo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Akitoa hotuba wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Leonidas Gama amesema jumla ya watuhumiwa 1243 wa dawa za kulevya wamekamatwa katika
matukio 831 yaliyohusishwa kukamatwa kwa aina mbalimbali za dawa za kulevya
katika 2011/2012.
Aidha Mheshimiwa Gama amefafanua kuwa
katika kipindi hicho jumla ya kilogramu 224.3 za mirungi kg 14244.7 cocaine kg
7, na Heroine gramu 239 na
watuhumiwa kufikishwa katika vyombo mbalimbali vya sheria.
Mheshimiwa Gama ametaja kuwepo kwa Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA na mpaka wa nchi jirani ya Kenya , Mkoa wake umejikuta ukiingia katika
changamoto za kupambana na tatizo hilo
la dawa za kulevya.
Katika kuhakikisha sheria inachukua mkondo
wake Gama, amesema tayari jumla
ya kesi 760 zimefungiliwa mahakamani, kesi182 zikiwa zimeshughulikiwa na kutolewa
hukumu huku kesi 572 zikiwa
katika katua mbalimbali mahakamani.
Mwenge wa uhuru umeingia Mkoani Kilimanjaro
tarehe 31/07/2012 ukitokea Mkoa wa Manyara ambapo unatarajiwa kukimbizwa katika halmashauri zote
saba zilizomo katika Mkoa huo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo mwenge wa uhuru,
umeanza kukimbizwa Wilaya
ya Same na baadaye kukabidhiwa
Wilayani Mwanga ambapo
utapokewa na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijjiini.
Utakapomaliza kukimbizwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijini Mwenge wa Uhuru utaelekea Wilayani Rombo
ambapo watakabidhi kwa uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Aidha Halmashauri ya Manispaa hiyo
itakabidhi kwa uongozi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Hai ambapo wataukabidhi katika Wilaya ya Siha kabla ya kuukabidhi
mwenge huo kwa uongozi wa Mkoa wa jirani wa Arusha.
Ukiwa Mkoani Kilimanjaro mwenge wa uhuru
unatarajia kufungua, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi
mbalimabli ya maendeleo ipatayo51
yenye jumla ya zaidi ya Tsh bilioni 4 ambayo imetokana na vyanzo
mbalimbali vya fedha .
Akielezea mchanganuo wa gharama za miradi
hiyo Mheshimiwa Gama amesema Serikali kuu imechangia Shilingi 2,032,599,724/=,
Halmashauri za Wilaya 455,295,775/=, Michango na Nguvu za wananchi
705,062,381/= huku wahisani na wafadhili wakichangia shilingi 892,470,710/=.
No comments:
Post a Comment