Wanahabari wakiwa makao makuu ya jeshi la Polisi wakimsubiri DK Slaa wa Chadema. Lakini Askari walitaka kutufukuza tukawagomea. lakini wakiwa na mambo yao wanatutafuta kila tulipo ili tuje hapa.
Ahahaaa picha hii ilinichekesha sana. Huyu jamaa aliyewekeka mkono namjua kwa jina moja tu la Hassan, nilikuwa nae chuoni TSJ baadae akapata kazi Mwananchi Communication akiwa mpiga picha. Na sasa amepata ajira jeshi la Polisi. Nilipotaka kumpiga picha akakataa na kukasirika sana. Wapiga picha wenzie wakamcheka sana kuwa yeye alikuwa akipiga watu picha leo hii yeye hataki.... Pembeni yake mwenye shati la ugoro ni jembe hilo anaitwa Mkinga Mkinga, pia tulikuwa pamoja TSJ na sasa ni mwandishi nguli wa The Citizen.
No comments:
Post a Comment