Malawi imekataa
kuitikia wito wa Tanzania kutaka isimamishe shughuli za kutafuta mafuta na gesi
ziwa Malawi, wakati suluhu ya mvutano wa mpaka ikisubiriwa.
Mvutano wa maneno umezuka kati
ya nchi hizo mbili baada ya Malawi
kuipa leseni Kampuni ya Uingereza kufanya utafiti katika eneo hilo .
Maafisa nchini Tanzania
wanasema mvutano huo uliodumu kwa miaka 50 sasa unaweza kuwa mkubwa iwapo
ugunduzi wa mafuta na gesi utatokea kwenye ziwa hilo
linalojulikana kama Ziwa Nyasa nchini Tanzania .
"Hili
ni suala nyeti sana na tungependa litatuliwe kwa
maelewano, tutaendelea na mazungumzo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania
alisema.
Membe
wiki iliyopita alviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa "shughuli za
uchimbaji katika eneo la kaskazini mashariki mwa ziwa hazina budi kusitishwa
kupisha mazungumzo kutatua mzozo huo yafanyike."
Msumbiji
pia inadai ina sehemu yake katika ziwa hilo
la tatu kwa ukubwa barani Afrika.
Mwezi Septemba mwaka jana serikali ya marehemu Bingu wa iliipa leseni kampuni ya Surestream Petroleum, kutafiti mafuta na gesi ziwani.
Mwezi Septemba mwaka jana serikali ya marehemu Bingu wa iliipa leseni kampuni ya Surestream Petroleum, kutafiti mafuta na gesi ziwani.
Mataifa
hayo mawili yatafanya mazungumzo juu ya mpaka kaskazini mwa Malawi katika
mji wa Mzuzu Agosti 20 mwaka huu.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment