Asalam allaykum ndugu zangu,
Futari yetu ya leo kama kawaida itakuwa ya harakaharaka ili kuweza kuwasaidia wale ambao hawana muda wa kukaa chini na kupika mapochopocho.
Leo tutafuturu marunda tu, naam matunda tu na protini kiasi.
tafuta matunda ya aina tano, si lazima ufuate kama nilivyoandika mimi ila hakikisha tu umepata matunda ya aina tano. Maembe, Nanasi, Papai, Ndizi mbivu, na Parachichi (avocado).
Ni vema ukipata na mayai ya kuchemsha na maziwa matupu bila sukari wala rangi. Hiyo itakusaidia kujenga afya na kupunguza vitu vya wanga katika mwili. Siku njema.
No comments:
Post a Comment