Zaidi ya watoto milioni moja wako katika hatari ya kupata
utapiamlo katika ukanda wa Sahel Afrika
Magharibi kwa mujibu wa wa mashirika mawili ya kiraia.
Shirika la World Vision na Save the Children yanasema mamilioni
ya familia wanahangaika kwa kile kinachoelezwa kuwa ni athari kubwa ya ukosefu
wa chakula.
Wanasema sababu kubwa ni ukame au upungufu wa
chakula, lakini pia hakuna uhakika wa chakula kutokana na bei kubwa ya chakula.
Mashirika
hayo yanataka uwekezaji zaidi kwenye chakula.
Hata
inapokuwa ni mwaka wa kawaida vifo 200,000 vya watoto vinawza kuhusishwa moja
kwa moja na utapiamlo,’ walisema.
Ukanda
wa Sahel ni eneo kame linalojumuisha pia Mauritania ,
Mali , Niger , Burkina
Faso , Senegal
na Chad .
Zaidi
ya watu milioni 18 katika eneo hilo
kwa sasa wamekubwa na njaa, mashirika hayo yamesema.
Mkurugenzi
wa masuala wa dharura wa World Vision Paul Sitnam alisema: "Watu maskini
kabisa …kimsingi hawawezi kupta chakula chochote sokoni kwa sababu ya ufukara
wa muda."
Alisema
tatizo haliwezi kutatuliwa kwa kugawa tu chakula, na jumuiya ya kimataifa
inahitaji kupeleka msaada wa haraka katika maeneo yaliyoathiriwa kuweka urahisi
w wa kukabiliana na ‘mtikisiko’ huo.
"Kuhakikisha
pia kuwa kuna muungano wa kifamilia, miundo mbinu na usalama wa kijamii kutoa
uangalizi kwa watoto na familia zao wakati wa mgogoro kama
huu " alisema.
Upungufu
wa mazao, kupanda kwa bei za mazao na uhaba wa chakula katika nchi jirani
kunachangia kuwa na tatizo sugu, Save The Children linasema.
Mwezi
Januari, Oxfam na Save the Children yalisema maelfu ya watu katika Pembe ya
Afrika walikufa kwa njaa mwaka jana kwa sababu jumuiya ya kimataifa ilishindwa
kutoa onyo mapema.
Mkurugenzi
mkuu wa Shirika hilo
Justin Forsyth, anatoa wito wa kujadili hili katika "mkutano wa
njaa", unaotarajiwa kufanyika baada ya michezo ya Olympic London.
Viongozi
wa Dunia, wafanyabiashara wakubwa, mashirika yasiyo ya kiserikali na
wanaharakati wa maendeleo watahudhuria mazungumzo katika siku ya mwisho ya
michezo.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment